ZAWADI YA PEKEE KUTOKA KWA MUNGU
Ndani ya jamii zetu kumekuwepo na watu nambao umri wao umepita umri wa kawaida wa kuingia katika ndoa, wakijulikana kama waseja. Je hii ni laana au inapelekea kuto kukubalika katika jamii na mtu kuonekana nasiyefaa? Majibu yake yanapatikana katika kitabu hiki. Kuna mambo ambayo yameonekana yakifanywa na watu kukidhi haja zao za kimapenzi, na kuyachukulia kuwa ya kawaida kabisa, pasipo kujua kuwa yote hayo yana kwenda kinyume na makusudi ya Mungu katika ndoa. Mambo hayo ni kama vile uzinzi, mitala, talaka na mapenzi ya jinsia moja.
Mke na mume wote katika ndoa wana
majukumu na wajibu wa kujenga na
kuboresha mahusiano bora ya ndoa ambapo
kuzaa na kulea watoto katika ndoa ni kusudi
lingine la Mungu la kuendeleza uumbaji. Kwa
vijana ambao mara nyingi wamekuwa na
changamoto za kutaka kufahamu ni mbinu
gani wazitumie katika kuingia kwenye
uchumba na baadae ndoa, kanuni kuu za
Kibiblia zimetolewa ili kukuongoza namna ya
kuingia katika ndoa kwa kufuata utaratibu
unaokubalika.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza