Yusufu Nina Ndoto
Je, upo tayari kuishikilia ndoto yako hata kama hakuna anayeona uwezo ulionao?
Je, upo tayari kuishikilia ndoto yako hata kama hakuna anayeona uwezo ulionao? Je, upo tayari kuhakikisha ndoto yako inakamilika hata kama wazazi wako, ndugu zako na hata marafiki zako wa karibu wanasema hauwezi kufika popote? Tatizo kubwa linalosababisha watu wengi kuachana na ndoto zao ni kusikiliza sauti za watu wengine kuliko sauti zao za ndani. Watu wanaweza kukuchukulia poa, lakini wewe ukianza kujichukulia poa tatizo huanzia hapo. Familia ya Yusufu haikuamini katika ndoto zake, lakini yeye alijiamini. “Kila ndoto huanza na yule anayeiota. Kila mara kumbuka kuna nguvu ndani yako, uvumilivu na kiu ya nyota za kuibadili dunia.” (Harriet Tubman). Usikubali hata siku moja ndoto yako izimwe ghafla kama mshumaa. “Kinachonihamasisha ni wale watu wanaoniambia hauwezi kufanya kitu fulani. Tafadhali niambie siwezi kufanya kitu fulani,” (Darren Hardy). Yusufu alihamasishwa na maneno ya ndugu zake. Maneno ya wanaokukatisha tamaa yakupe hasira ya kutimiza ndoto zako na wala si kurudi nyuma.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza