Yaliyonikuta Tanga
Price:
10,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Jan 04, 2021
Product Views:
1,888
Sample
SIMULIZI YA KUSISIMUA!
UTANGULIZI
Wakati Musa anaianza safari yake ya kutoka Arusha kwenda Tanga, aliamini yale yote aliyoambiwa na rafiki yake Maliki kuhusiana na uzuri wa mji huo pamoja na watu wake.Mabinti wa kitanga na ufundi wao wa mapishi, ulaini wa lugha yao, ujuzi wa mapenzi na uwiano asilia kati yao na neno PENZI.
Simulizi za kubebwa mgongoni huku ukiandaliwa maji vuguvugu ya kuoga yenye harufu nzuri ya hiliki, zilijirudia mara kwa mara mawazoni mwake kadiri anavyolisogelea jiji hili la bandari ya Kaskazini mwa Tanzania. Hii ni fursa ya kuyashuhudia.
Akiwa Tanga Musa aliyejaa na matamanio ya kupata raha za mapenzi ya ki-Tanga anakutana na Zuhra katika klabu moja maarufu ya usiku ya Lacasa Chica.
Matumaini ya Musa yanapotea ghafla! Maskini, hakujua kama alikuwa katika mtego mkubwa uliogubikwa na dhana potofu zilizopelekea ajutie yanayomkuta baada kukutana na binti huyo mwenye asili ya kiarabu.
Fuatilia kisa hiki kinachosimuliwa na Mohammed Hammie Rajab, mtoto wa aliyekuwa gwiji la uandishi Tanzania marehemu Hammie Rajab ili ujue ni yapi YALIMKUTA Musa akiwa Tanga.