YAFAHAMU MAMBO 4 YANAYOWAGHARIMU VIJANA
Kusudi la kuumbwa kwako kijana,matumizi yako ya Muda leo, Aina za marafiki ulionao, Na nidhamu yako ya Fedha inaamua Maisha yako ya uzeeni yawe vipi!
Ni ukweli usiopingika kwamba wako vijana ambao kwa kweli ukiyatazama maisha yao unatamani kuwa kama wao kwasababu ya matokeo wanayoachilia kwenye jamii na Taifa kwa ujumla, ila hawakosekani vijana ambao bado wanahangaika na kukimbizana na mifumo ya dunia hii ilimradi tu wasionekane wapo nyuma sana.
Na ubaya ni kwamba katika mchakato huo wa kukimbizana na mifumo ya dunia hii wamejikuta wakipoteza uhalisia wao na kuishi maisha ya ajabu sana, yaani imewagharimu wengine hata kupoteza uhai.
Sasa ndani ya kitabu hiki nimekuandikia mambo manne ambayo kwa hayo vijana wengi yamewagharimu sana na yamewafanya wengine mpaka leo washindwe kujua muelekeo wa maisha yao.
Nimeyagawa mambo hayo katika sura 4 tu. Utakutana Na hatari za kutokuweka Akiba ukiwa KIJANA, kutokujua Kusudi la kuzaliwa kwako, madhara ya kutumia Muda wako Vibaya ukiwa KIJANA,Na Aina za marafiki zinavyoweza kuathiri Maisha yako.
Kitabu Ni kifupi, lugha yake inaeleweka Na hutachoka kukisoma!
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza