WEWE NI BIDHAA YA MUNGU
Tambua ulichoumbiwa, kiishi, mafanikio yatakufuata.
Bidhaa yoyote ile hutengenezwa kwa lengo mama la kwenda kutawala soko na kutoa suluhisho la matatizo yanayowakabili watu. Na hii ndio kiu na furaha ya mtengenezaji wa bidhaa husika.
Hata kwetu binadamu, lengo la kuwepo hapa duniani kama bidhaa ya Mungu ni KULITAWALA SOKO (dunia) na kutatua changamoto mbalimbali kupitia karama na vipawa tulivyopewa na Mungu. Mwenyezi Mungu kama muumba wetu anajisikia furaha kuona tunafanikiwa.
Hivyo kitabu hiki cha \\\"WEWE NI BIDHAA YA MUNGU\\\" ni maalumu kwa ajili yako wewe uliye na kiu ya kulitawala soko kupitia karama na vipawa ulivyopewa na mwenyezi Mungu.
Ukweli ni kwamba hautaishi duniani milele, ila unayo nafasi ya kufanya jambo litakaloishi milele kwa niaba yako pale utakapokuwa umeondoka duniani.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza