WEKEZA KATIKA ELIMU YA MWANAO
Katika ulimwengu wa leo asilimia kubwa ya wazazi au walezi wanaelewa umuhimu wa eliimu kwa watoto wao, lakin ni wazazi wachache wanaoelewa maana na umuhimu wa kuwekeza katika elimu ya watoto wao ipasavyo kuwekeza Katika kitabu hiki mzazi utapata maelezo yatakayokupa mwanga pindi unapokuwa umedhamiria kuipa kipaumbele cha kwanza elimu ya mwanao. Kitabu hiki kitakupa mifano na maelezo rahisi kueleweka itakayokuonyesha namna unavyoweza kushughulika na taaluma ya mwanao, maelezo haya yameletwa kwa lugha nyepesi kueleweka hata na mzazi mwenye kiwango kidogo cha elimu, hivyo inabaki ni jukumu la mzazi mwenyewe kujisomea kitabu hiki na kujiongezea maarifa.\r\nKitu cha muhimu unachotakiwa mzazi kukumbuka ni kwamba kuyafahamu mambo yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki bila kufanyia kazi kwa vitendo hakuna faida yeyote. Mwisho nawatakia wazazi na walezi wote kila la kheri katika malezi ya watoto wenu kwani jukumu la malezi ni zito na linahitaji kuwa na hekima, busara, maarifa na uvumilivu wa kutosha pamoja na kuomba siku zote kudra za MUUMBA.
Kitabu hiki kimewalenga wazazi, wazazi watarajiwa pamoja na walezi
Kitabu hiki kitakupa mbinu mbalimbali ambazo ukiziweka kwenye vitendo zitasaidia sana kumjenga Mwanafunzi kitaaluma. Hivyo wazazi na walezi mnaombwa kujifunza mbinu mbalimbali zinazopatikana ndani ya kitabu hiki na kuzitia katika vitendo.