We' Kuweza?
Kupenda mtu asiyependeka ni kitu cha hatari! Mama Sabrina kimemkuta kitu!
Mama Sabrina mjasiriamali anajikuta kitanzini mwa mikono ya sheria baada ya kupigana na kimada wa mumewe na kupelekea umauti wake. Anahukumiwa kwenda gerezani kwa kipindi cha miaka thelathini lakini anatoka kwa msamaha wa rais baada ya miaka kumi. Anarudi nyumbani anakuta mambo ni tofauti na alivyoyaacha. Ikawa bora ya jana kuliko ya leo. Mikasa mingi inafunguka kadiri anavyoendelea kuishi uraiani.
Mama Sabrina, anafanya kila awezalo kuhakikisha anabaki imara kama mwanamke wa shoka licha ya husda, fitna na majaribu mbalimbali kutoka kwa mumewe. Mwandishi ameendelea kutuletea visa na mikasa ya Uswahilini. Katika riwaya hii, amekusanya mtiririko wa visa vya kusikitisha na vitakavyokufanya ushindwe kukiweka kitabu hiki chini.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza