WAKATI UNASUBIRI
Miaka ya usingo si miaka iliyolaaniwa bali ni miaka ambayo Mungu amekupa kama zawadi ili utengeneze kesho yenye hatma njema.
Ndoa ni ya maana sana kwenye maisha ya mwanamke yoyote lakini ndoa si kila kitu . Mtu hapati thamani kwasababu tu ameolewa bali dunia humpa thamani mtu kwasababu ya thamani aliyoileta kwenye maisha ya wengine.
Ukitaka kuthaminika kwenye huu ulimwengu lazima uhakikishe kuwa umegusa maisha ya watu na kufanyika majibu kwenye matatizo yao.
Na hauwezi kuwa na majibu ya matatizo ya watu kama usipoishi ndnai ya kusudi la maisha yako,ndio!Kusudi la maisha yako ndilo limebeba kila kitu kuhusu wewe na watu wanaokuzunguka.
Badala ya kuhangaika kutafuta mwanaume wa kukuoa kama binti hakikisha jambo la kwanza unalopambana kulipata ni kuishi ndani ya maisha Mungu aliyokukusudia yaan maisha ya kusudi.
Ndoa inaweza ikawa chanzo cha mafanikio yako ama la kulingana na uchaguzi utakaoufanya wakati unasubiri lakini jambo ambalo haliwezi kukusaliti kamwe ni maisha ya kusudi maana kadiri utakavyopambana ndivyo milango itakavyofunguka zaidi kwa ajili yako.
Binti na mwanamke ambaye haujaolewa bado hakikisha wakati huu wa kusubiri unajenga misingi bora itakayokufaa sasa na kesho.
Hakikisha unajua thamani yako na kuilinda,simama kwenye nafasi yako ,kuwa mtu unayemtumikia Mungu,fanya kazi kwa bidii na tengeneza misimamo yako itakayokuongoza kwenye maisha yako.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza