Wahuni Wote Peponi
Mambo ya ndoa za mitala imepelekea mtu kuikimbia nyumba yake mwenyewe na kurudi kwao Buza kwa Lulenge bila kupenda. Anakutana na sahib wake wa utoto, wanarudia maisha ya mtaani. Punde anaingia wazimu wa kutaka kujaribu maisha ya kujinufaisha kwa kile ulichopewa na mama. Yaliyomkuta! Aibu!
Sijali ni mwanamama anayepita mambo magumu katika maisha yake. Kubwa ni la kupewa talaka na kurudi nyumbani kwao Buza kwa Lulenge. Baya kupita hilo la talaka ni kukutana na mtu aitwaye Mzeta Salum Keita! Kiumbe kilichojawa na falsafa za ajabu shida zako mtaji wangu, nipe nikupe, sina msaada kama hujisaidii.
Mwandishi amejipambanua katika kuandika riwaya za vituko Uswahilini. Hii ni riwaya yake ya kwanza yenye kuonesha balaa la watoto wa BUZA!
Sasa ukitaka kujua WAHUNI wanaingiaje PEPONI humu jibu linapatikana!