VISASI NA RISASI
Riwaya ya kusisimua
VISASI NA RISASI
Akiwa amejiridhisha pasipo shaka, Julius Mabala anaitisha mkutano wa wanahabari kuibua kashfa nzito ya ufisadi ya mabilioni ya shilingi; kashfa inayomgusa kigogo aliye na ndoto ya kuusaka uongozi wa juu kabisa wa nchi. Julius anaugua ghafla akiwa mkutanoni na anaaga dunia kabla hajatimiza azma yake.
Noela Kuzi, mjane wa marehemu, akiwa mbele ya kamera ya televisheni wakati wa mazishi ya Julius, anatoa tamko linalowatia kiwewe wauaji. Naye hayupo salama. Siku chache baadaye, akiwa safarini, gari lake linahusika katika ajali ya kupangwa. Waliopanga tukio hilo wanaamini kuwa wamemmaliza. Kwa miezi kadhaa anatibiwa hospitalini huku madaktari wakiwa wamekata tamaa, lakini kama muujiza afya yake inaimarika.
Anaporejea anakuwa na jambo moja tu kichwani—kuwafichua wahusika wote. Harakati zake zinazaa visasi; na visasi vinasababisha risasi kutafuna roho za watu. Mwishowe inakuwa visasi na risasi