UZURI WA GEREZA Hazina Iliyo Sahaulika
Nilibahatika kuingia gerezani na kujikita katika kufanya upelelezi wa kisiri ndani ya gereza kuu la Butimba Mkoani Mwanza hapa nchini Tanzania kwa muda wa siku 60 mfululizo, kitendo ambacho ni hatarishi kwani kinapingana na sheria za Jeshi la Magereza. Matokeo ya upelelezi huo yaliniibulia taarifa sahihi zilizo baini kuwa gerezani kuna hazina ya thamani ya siri za Mungu!
Kitabu hiki Uzuri wa Gereza; Hazina Iliyo Sahaulika - Sehemu ya Kwanza, kinakufunulia hazina hizo za thamani zilizo hifadhiwa na Mungu kimaalum nakwa usiri mkubwa ndani ya gereza la serikali, ambazo ni chachu ya UAMSHO wenye kuleta mapinduzi ya kiroho, kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kiujasiliamali kwa kupitia katika rasilimali watu.
Wewe unayejiona uko huru nje ya gereza la kiserikali, nakutangazia kuwa inawezekana kabisa kuwa umefungwa katika gereza la utandawazi wa kidunia kwa vifungo vya muda maalum, vifungo vya maisha na kusubiria kunyogwa hadi kufa kwako. Mungu kwa mapenzi yake ameamua kukukomboa ili uwe huru nje ya gereza hilo kupitia katika utandawazi wa maendeleo endelevu ya kiroho kwako binafsi na taifa lako kwa ujumla ili kujitawala kifikira na kuutawala ulimwengu unaokuzunguka kwa uhuru.
Maudhui ya kitabu hiki yana thamani kubwa kwa vile yanakutiririkia sambamba na shuhuda za maisha halisi niliyoyapitia mimi mwandishi na shuhuda nyingine za watu mashuhuri hapa ulimwenguni ili kukifanya kuwa muhimu katika kuhuisha roho yako na kufikirisha akili zako binafsi uweze kujitafuta, kujipata, kujitathimini na kutengeneza chapa yako iliyo bora na mpya tofauti na ulivyo sasa kabla ya kusoma kitabu hiki.
Usipange kutokukisoma kitabu hiki, kwani ni ufunguo wa kufungulia mlango wa hatima njema ya maisha yako binafsi na hatima njema ya taifa lako!