UTAWALA WA MUNGU NA SERIKALI ZA KIDUNIA
UTAWALA WA MUNGU NA SERIKALI ZA KIDUNIA
Katika dunia hii kuna wabobevu wa maarifa na ujuzi juu ya mambo mengi yanayoiendesha mifumo ya maisha. Mambo hayo yakiwepo Sayansi kwa upana wake na maarifa yanayohusu mahusiano na mengineyo mengi. Watu wengi waliojikita katika nyanja hizo, wamehesabika kuwa wabeba hazina za maarifa na kupewa heshima na tuzo katika jamii. Hiyo ni haki kwao kutokana na yale waliyobeba kuwa sehemu ya manufaa kwa jamii na duniani kwa ujumla. Lakini mkononi mwako umeishika hazina ya maarifa ya rohoni. Kitabu hiki kimebeba mambo muhimu yahusuyo mifumo ya serikali za kidunia. Historia na mambo yajayo yakiwepo; dhiki kuu, vita ya Har-Magedon, Utawala wa Kristo wa miaka 1000 pamoja na Gogu na Magogu katika vita kuu ya nne ya dunia. Kuyapata maarifa haya ni jambo la kupongezwa kwani ndio pekee yaliyobeba hatima ya maisha yako na viumbe vyote vilivyoko katika ulimwengu huu. Hongera kwa kujipatia nakala yako.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza