Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Utatu Katika Biblia - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

UTATU KATIKA BIBLIA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
5,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Mar 15, 2024
Product Views:
370
In category:
Sample

Kitabu hiki kinashughulika na masomo kama vile: Mgawnyiko wa imani kuhusu utatu wa Mungu; maandiko yatumikayo kufundishia utatu kimakosa; sura ya Mungu ni ya namna gani; tofauti ya kujifunua kwa Mungu katika Agano la kale na Agano jipya; maana ya majina matatu ya Mungu; majina ya Mungu katika Agano la kale na Agano jipya, n.k. Ni matumaini yangu kuwa utakuwa mwaminifu kufuatilia maandiko yaliyotumika katika masomo haya yote, bila kujali itikadi za kidini au imani.

Dibaji\\r\\n

Namshukuru sana Mungu kunipa nafasi hii muhimu ya kushirikisha ufunuo mwingine wa \\r\\nMaandiko matakatifu, kwa watu wote wanaopenda kusoma na kulielewa Neno la Mungu. Mimi \\r\\nnafikiri hii ni njia moja ya kuujenga mwili wa Kristo, ambao sisi ni viungo vya mwili huo. Kwa \\r\\nkawaida watu wanaopendana katika jamii, hupenda kushirikiana katika mambo yote yaliyo \\r\\nmema hata yaliyo mabaya pia.

Huduma yangu ya kufundisha Biblia kwa muda wa miaka zaidi ya ishirini, ikiwemo ya huduma \\r\\nmashuleni pamoja na chuo cha theolojia ya Biblia, imenipa uzoefu mkubwa wa kukutana na \\r\\nmaswali kutoka kwa watu mbalimbali na itikadi mbalimbali; ambayo hayajibiki kwa kutumia \\r\\nmajibu yanayotokana na imani za madhehebu. Lakini Biblia inapotumika kwa kujitegemea \\r\\nyenyewe na kanuni zake, bila kuingiza itikadi zetu, ina uwezo wa kujibu maswali yote kwa \\r\\nuthibitisho mkubwa!

Katika kitabu kingine kiitwacho “KANUNI ZA KUFASIRI BIBLIA” nilielezea kwa kirefu sana \\r\\njinsi ilivyo muhimu kusoma Biblia kwa kutumia “KANUNI” zake. Kukosa kanuni hizo, \\r\\nkumesababisha kuwa na migongano mingi sana katika kuifasiri Biblia, na mwili wa Kristo \\r\\nkugawanyika kiimani hata kudharauliana sisi kwa sisi, kila mmoja akimhesabu mwenzake kuwa \\r\\namepotoka kwa kunyosheana vidole. Imeonekana kuwa kutokana na hali, hakuna awezaye \\r\\nkumsaidia mwingine! Je, kanisa la Yesu litaendelea na mwendo mpaka lini?\\r\\n

Kwa mara nyingine tena, katika kitabu hiki kiitwacho, “UTATU KATIKA BIBLIA” \\r\\nnimekiandika kwa kusudi la kuwafahamisha watu wote, Biblia isemavyo kuhusu utatu wa \\r\\nMungu, kwa kutumia KANUNI ZA KUFASIRI BIBLIA, ili kuweka wazi mambo ambayo \\r\\nyanafundishwa na kuaminiwa kwamba, yapo katika Biblia au la! Kuna mambo yanayotakiwa \\r\\nkusisitizwa lakini yanapuuzwa; na yale yasiyo na umuhimu yanasisitizwa sana!

Kitabu hiki kinashughulika na masomo kama vile: Mgawnyiko wa imani kuhusu utatu wa \\r\\nMungu; maandiko yatumikayo kufundishia utatu kimakosa; sura ya Mungu ni ya namna gani; \\r\\ntofauti ya kujifunua kwa Mungu katika Agano la kale na Agano jipya; maana ya majina matatu \\r\\nya Mungu; majina ya Mungu katika Agano la kale na Agano jipya, n.k.\\r\\nNi matumaini yangu kuwa utakuwa mwaminifu kufuatilia maandiko yaliyotumika katika \\r\\nmasomo haya yote, bila kujali itikadi za kidini au imani. Mungu akubariki! 

More Products On Discount
More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
Old is Gold