USIPOTEZE TUMAINI
USIPOTEZE TUMAINI rnNyakati ngumu katika maisha huja na kuondoka huwa hazidumu.rnrnKama ambavyo mti huwa unakubali kupoteza majani yote kipindi cha kiangazi ili kuweza kujiimarisha zaidi kwenye siku za usoni.rnrnNdivyo ambavyo maisha yanavyoenda kuna majira lazima upitie ambayo yatakufanya upoteze biashara yako, kazi yako, marafiki zako wa karibu au ndugu kabisa au upoteze mahusiano yako na mchumba wako uliyempenda sana.rnrnHaya ni majira ya joto yanapomfika mtu, lakini pamoja na nyakati hizi bado kuna kustawi tena mbeleni kwan kuna nyakati njema sana zinakusubiri kwa shauku.rnrnKumbuka hakuna chumba cha giza kama nuru ipo.rnrnHaijalishi umeanguka mara ngapi Inuka tena katimize ndoto zako, maelfu na maelfu yanakusubiri wewe.
Kwenye Ulimwengu tulio nao unahitaji kujitia moyo mara tisa kabla mtu mwingine hajakutia moyo.
Hii ndiyo sababu nikaandika mbinu zitakazo kuwezesha kuwa na furaha wakati wengine wamekukatia tamaa.
Mtu mmoja akasema “Usimkatie tamaa binadamu anayeishi haijalishi ni maisha gani anaishi ila kwa sababu anaishi usimkatie tamaa”.
Watu wanaweza kukukatia tamaa ila kamwe usijikatie tamaa, kwa sababu hakuna anayejua yatakayozaliwa ndani ya dakika moja.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza