USIONDOKE HARAKA DUNIANI BADO MUNGU ANAKUHITAJI
Usiondoke haraka duniani ni kitabu kinachoeleza umuhimu wa uwepo wako duniani kwa Mungu, watu wengi linapofika suala la kuondoka duniani ama kupoteza wapendwa wao hupata maumivu Sana lakini ukweli ni kuwa Mungu anaumia zaidi juu ya kifo cha MTU yeyote ambaye anakua ameondoka duniani bila ya kukamilisha mapenzi au makusudi ya Mungu duniani. Mungu alitoa angalizo mapema juu ya kifo hii no wazi hakutaka MTU akae duniani kwa muda mfupi Bali Alitaka adumu milele duniani. Kwa bahati mbaya kina watu hawafikishi hata nusu ya miaka yao waliyopaswa kuishi duniani.Kitabu hiki kitakusaidia kupata maarifa ya kuweza kuishi miaka unayopaswa kuiishi hapa duniani. Shetani anatamani watu wajue kuwa vifo vyote vinavyotokea duniani ni mpango wa Mungu lakini si kweli hata Hivyo tangu mwanzo kifo halikuwa kusudi la Mungu.
Katika kitabu hiki utajifunza ni kwanini Mungu hataki watu waondoke haraka duniani? Kifo ni nini? Kifo cha mapema ni kipi? Kifo kinatokeaje? Mambo kumi yanayosababisha kifo cha mapema, ufanye nini ili kukishinda kifo cha kabla ya wakati wako? Namna ya kuishinda roho ya mauti, kuumwa sio kufa n.k
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza