Usimamizi Wa Uwekezaji Kwenye Ardhi Na Majengo
Namna Ya Kuongeza Kipato Kwenye Majengo Ya Kupangisha
Hiki ni moja ya vitabu ambavyo nimeviandika kwa namna ya pekee sana. Miongoni mwa mambo utakayojifunza kwenye kitabu hiki ni kama ifuatavyo;-
Moja; Aina ya usimamizi wa uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Mbili; Bima za majengo.
Tatu; Makundi ya majengo kulingana na ugumu wa usimamizi wake.
Nne; Maana wa wapangaji/mpangaji bora.
Tano; Jinsi ya kupata wapangaji bora.
Sita; Jinsi ya kufanya makadirio ya kodi ya upangishaji wa nyumba.
Saba; Asilimia unayotakiwa kutengeneza kila mwezi na mwaka kutoka kwenye nyumba za kupangisha.
Nane; Wanatimu wa muhimu sana na wanatimu wa ziada kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo.
KUMBUKA; Utaweza kufahamu mambo ya msingi kuhusu soko mahalia la majengo ya kupangisha. Kwa ujumla, soko mahalia ndicho kitu ambacho huathiri uwekezaji kwenye majengo ya kupangisha.
Pakua (download) kurasa za mwanzo wa kitabu hiki ili kujifunza sehemu ya maarifa na uzoefu ulioandikwa kwenye kitabu hiki.
Rafiki yako,
Aliko Muda.
Mbobezi wa ardhi na majengo.