Usiku Wa Deni
Usiku Wa Deni
Hallow! Naongea na Dokta Malik?" Ilisikika sauti nzito ya mtu wa upande wa pili. Kabla hajajibu, Dokta Malik alisita. Asingeweza kujitambulisha kwa mtu asiyemfahamu. “Hallow!” Mtu yule aliita tena. “Naongea na nani?" Dokta Malik aliuliza huku akipambana na usukani wa gari. "Nina hakika sijakosea namba, na najua umetoka kazini tayari. Umeshafika nyumbani kwako?" Yule mtu aliyeonekana kukwepa kujitambulisha aliuliza tena. "Bado kama mita mia mbili ili nifike." Alilazimika kumjibu. "Nikusumbue ndugu yangu, rudi haraka kazini kwako, kuna kijana ameokotwa huko Lugubu…? “Lugubu?” Dokta Malik alishangaa maana ni mbali sana kufika mjini. “Actually sio Lugubu ila ni njia ya kutokea huko.” “Okay! Ana changamoto ipi?” “Sijui, wala sina hakika kama tayari ameshafariki ama mahututi." "Nafikiri ungemtafuta daktari aliyepo zamu sasa." "Sijakupigia kimakosa dokta!" "Kwa nini ni lazima niwe mimi?" "Kwa sababu ni wewe tu unaweza kumsaidia." Dokta Malik alishusha pumzi. Akapunguza mwendo na kwenda kuegesha pembezoni mwa barabara akiliacha likiunguruma. Endeleaaa…….!
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza