Usichoke Safari
Uwanja Mpya Wa Tenzi
Ushairi una historia kongwe sana inayoendelea kubeba hazina, utajiri wa lugha na pia kutunza utamaduni wa jamii husika. Ukongwe wake unaendelea kufanya kuheshimika ulimwenguni kote, kuanzia wagwiji wa kina William Shakespeare, na hapa nyumbani wakina Shabaan Robert, Amri Abeid Kaluta, Mnyampala na Saadani Kandoro. Ni fani ya pekee na yenye ufahari wa hali ya juu kwa jamii husika. Hekima iliyopo katika utunzi wa Mashairi na tenzi ni daraja la kuikomboa jamii, kuelemisha jamii na kuhamasisha kufanya Kazi. Licha ndani yake kuna burudani ziimbwapo kwa mahadhi ya sauti. Kutunza na kudumisha Kazi zao ni uzalendo mkubwa wa kuigwa na vizazi kwa vizazi.