USALITI WA KUAMINIANA
Mwanadamu siyo wa kumwamini. Wakati wowote anaweza kukuangusha.
USALITI WA KUAMINIANA; Hiki ni kitabu pekee kinachoelezea suala zima la usaliti katika jamii, usaliti katika kazi, mahusiano ya kimapenzi/ndoa, kibiashara na kifamilia. Kitabu hiki kina hadithi za kusisimua zinazosaidia kufundisha jamii ni kwa namna gani usaliti unavyoleta madhara makubwa katika jamii, ndani ya nyanja zote za maisha yaani kazini, mahusiano au ndoa, biashara na kifamilia.
Vilevile kitabu hiki ni tiba kwa wale waliosalitiwa katika maeneo tofauti, kwani kitawasaidia kuepukana na usaliti kwa mara ya pili na pia kupona kabisa na maumivu au madhara waliopata baada ya usaliti.
Mwisho kitabu hiki kimebeba mafundisho makubwa ambayo yatamsaidia msomaji kuishi vizuri na kupata mafanikio makubwa katika maeneo ya kazini, mahusiano au ndoa, biashara na familia kwa ujumla.