Urafiki Wa Okello Na Agaba Ni Balaa
Urafiki wa Okello na Agaba ni balaa
Okello na Agaba ni marafiki wawili wanaoishi Mjini Kampala. Okello kwao ni Kyoga, katikati kabisa na Ziwa Kyoga nchini Uganda, ukitazama ramani ya Uganda, hapo kwa akina Okello ndio katikati kabisa ya nchi yao. Agaba ni mtoto moja mtundu sana kama alivyo rafiki yake Okello. Ila yeye anatoka Mjini Mbarara, kijiji chao kinaitwa Utunduni. Wao wako karibu zaidi na nchi ya Tanzania mahala palipozaliwa Kiswahili, lugha moja safi sana na tamu mno mdomoni ukiongea. Okello na Agaba wamekutana Mjini Kampala, Kampala ni mji mkuu wa nchi yao Uganda kama vile Nairobi ni mji mkuu wa Kenya, Dodoma ni mji mkuu wa Tanzania na Kigali ni mji mkuu wa Rwanda. Endelea........!