UNAJUA ASILI YA TABIA ZAKO?
Hali Ya Maisha Yako Inachangiwa Na Silika Yako
Umewahi kulaumiwa na mtu kwamba una tabia ambayo haipendi wakati wewe unajiona upo sawa kabisa? Umewahi kumshangaa mtu mwingine kwa tabia yake ambayo pengine unatamani ungekuwa nayo lakini unaona kabisa kwamba huwezi kujifunza au kuiiga na kuifanya kwa ufanisi kama yeye?
Kuna watu wamekuwa wakigombana, kutukanana, kuumizana na hata kuuana na wapenzi au wenza wao kwa sababu hawakujua asili ya tabia zao wenyewe na asili ya tabia za wenza wao.
Kuna watu wamewafukuza waajiriwa wao ambao wangeweza kuwa watu wenye manufaa kwao. Kuna watu wamefukuzwa kazi kwa sababu hawakujua tabia za wakubwa wao kazini au hawakujua tabia zao vema. Kuna watu wengi wameshindwa kuchagua fursa za ndoto zao kwa sababu hawajui vema asili ya tabia zao na fursa zinazoendana na tabia zao. Ili uwe na amani na boss wako, soma kitabu hiki. Ili uweze kuchagua fursa sahihi inayoendana na tabia zako, soma kitabu hiki.
Ukisoma Kitabu hiki utaweza kujua vema asili ya tabia zako na kujitambua vema. Utajua kwa nini una tabia ulizonazo. Utajua pia kwa nini watu wengine wana tabia tofauti na za kwako na namna ya kuhusiana nao bila kuwa na ugomvi wa mara kwa mara. Utajua pia namna ya kuchagua mwenza mtakayeendana vema kitabia kama bado hujaingia kwenye ndoa. Kama upo kwenye ndoa tayari utajua tabia za mwenzako na jinsi ya kuishi naye kwa amani na upendo. Hiki ni kitabu kwa ajili yako na wale wote uwapendao.