UNABII WA DANIEL NA SIKU ZA MWISHO
Kitabu cha Danieli kiko miongoni mwa vitabu vya unabii mrefu, au manabii wakuu,ikiwa ni pamoja na Isaya, Yeremia na Ezekieli. Vimepewa majina hayo kutokana na sababu kuu mbili zifuatazo: a) Unabii wao mwingi unahusu kipindi kirefu, tangu wakati wao mpaka wakati wa Kanisa la Agano Jipya; b) Wao wenyewe kutabiri kipindi kirefu chini ya utawala wa wafalme kati ya watatu na wanne. Danieli Mwenyewe alifanya kazi chini ya utawala wa Nebukadreza, Belshaza, Dario na Koreshi.
DIBAJI.
Danieli ni mmoja wa manabii wakuu na wenye unabii mzito wa siku za mwisho. Sababu za kuitwa manabii wakuu, au manabii wenye unabii mrefu kwanza; ni kwa sababu walitabiri au kutoa huduma zao kwa muda mrefu, wakiwa chini ya wafalme wengi. Pili, unabii wao ulikuwa wa kutimizwa kipindi kirefu, yaani kuanzia muda wao mpaka siku za mwisho wa dunia. Wakati manabii wakuu wengine walitoa unabii wao juu ya mambo yahusuyo kanisa; Danieli alitoa unabii wake kuhusu kanisa, mpinga Kristo na siku za mwisho wa dunia.
Katika kipindi hiki tulicho nacho, kumetokea mafundisho mengi sana yanayochanganya imani za wakristo, hasa kuhusiana na matukio ya siku za mwisho; yaani kuja kwa Yesu mara ya pili, dalili zake na mwisho wa dunia. Mafundisho haya yanayoenea na kuwachanganya watu, zaidi yanatokana na kutokukielewa kitabu cha Danieli, na kitabu cha Ufunuo wa Yohana. Mafundisho haya hayazingatii kabisa unabii wa Danieli ambaye alipewa maono ya kutosha kuhusu siku za mwisho katika nusu nzima ya kitabu chake.
Ili kuwasaidia waamini wa madhehebu yote walio na shauku ya kuujua ukweli huu, nimekiandika kitabu hiki kwa kutumia kanuni muhimu za kusoma na kufasiri Biblia. Nakualika kukisoma kitabu hiki bila kujali itikadi za kidini, bali kukisoma ili kupata ukweli wa maandiko. Mungu hajawahi kuficha ukweli wa mambo hata watu wake wachanganyikiwe; lakini nalitangulia kutupa mpango wake na ratiba yake kwa matukio yote yatakayolipata kanisa mpaka wakati wa kuja kwa Yesu, ili tusifadhaishwe na mafundisho ya uongo hata kupotea.
Nakutakia Baraka za Mungu wewe msomaji wangu!
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza