UMUHIMU WA MPANGO BIASHARA
MUONGOZO SAHIHI KWA BIASHARA ZINAZOANZA NA ZILIZOKWISHA ANZA.
Kuna maswali mengi ambayo mfanyabiashara na mjasiriamali lazima ujiulize juu ya biashara yako unayotaka kuanzisha au inayoendelea, moja ya mambo hayo ni andiko la mradi wako. Unaweza jiuliza je, mradi wako una Mpango Biashara (Business Plan) au unafanya tu kibubu bubu? Kama unafanya kibubu basi jitafakari vizuri sasa.
Moja Kati ya wachawi wa Biashara yako ni andiko. Kumekuwa na maneno mtaani yasio sahihi juu ya maandiko mbalimbali ya biashara kuwa kinachoandikwa uwa hakina uhalisia na ukweli wenyewe. Jambo hilo sio sahihi, ukiona mtu anakwambia kuwa mpango biashara haikupi taswira kamili basi ujue mtu huyo hakufanya tafiti za kutosha juu ya biashara yake au aliemuandalia hakuwa makini au yeye mwenyewe hayuko makini.
Biashara yoyote kuifanya bila andiko ujue unategemea nimuujiza ndugu yangu. Kuna mtu atafikiri kuwa naongea hivi kwa lengo kuwa nikuandikie andiko, lahasha bali ninachojaribu kukuonyesha hapa ni kuwa jitahidi kabla ya kuanza biasha andaa andiko lako au kama ushaanza biashara jitaidi uandae andiko la mradi wako. Sio lazima tukuandalie sisi, unaweza tafuta mtu yeyote mtaalamu aliekaribu nawe unayemuamini akakuandalia au ukaandaa mwenyewe.
Andiko ni muhimu sana ndugu yangu mfanya biashara/mjasiriamali ambae unataka kufanya biashara yenye tija na endelevu. Ushawahi kujiuliza kwanini ukienda kuomba mkopo benki wanakuomba andiko la mradi? Au kwanini ukiomba msaada kwa wahisani wengine kwanini uomba andiko? Hii maana yake ni kuwa andiko utoa picha ya biashara husika ilivyo na itakavyokuwa mbeleni na mtu yeyote makini hawezi kwenda kinyume na andiko lake.
Wewe mfanyabiashara/mjasiriamali acha kufanya biashara kwa mazoea tu, andiko makini ukupa uhalisia na ukilizingatia upata uhalisia kwa 95%. Tuache mazoea. Kupitia kitabu hiki nahakika utajifunza mambo mengi mauri na yatakuwa msaada mkubwa kwako na utaacha kufanya biashara kimazoea.
Frank Alfred Ndyanabo,
Mkurugenzi Mtendaji
Nyumbani Business Plan Limited
+255785494456
+255753494456