
Umaarufu
UMAARUFU Maana, Kusudi, Faida JE, MUNGU ANAPENDA UWE MAARUFU?
Dr Myles Munroe aliwahi kusema when purpose is not known abuse is innevitable ikimaanisha kuwa kama kusudi la kitu chochote halijulikani basi kutumiwa vibaya hakutaepukika, Ndivyo ilivyo kwa umaarufu huchukuliaa katika mtazamo hasi kwenye jamii kwa vile jamii inakosa uelewa wa kujua njia sahihi za kuwa maarufu, maana ya umaarufu faida zake, kusudi lake na hata mtazamo wa kiimani kuhusu umaarufu, Katika jamii siyo rahisi mzazi, mwalimu hata kiongozi wa kiroho kuhimiza watu kuwa maarufu, jamii kwa kiasi kikubwa huchukulia umaarufu katika mtazamo hasi. Ndivyo ilivyo kwa wengi walio maarufu kwa vile hawafahamu kusudi lake hujikuta wakiingia katika mkumbo, skendo na mitindo ya maisha isiyofaa hata baadhi yao kufilisikika na kuisha pabaya mfano bondia wa zamani Mike Tyson na beki wa arsenal Emmanuel Eboue. Kitabu hiki kinajadili kwa kina na kwa mifano kuhusu umaarufu na namna unaweza kutumika kwa faida, Na kinatoa mwanga kwako wewe kuwa mtu maarufu kwa vile itakuwezesha kukamilisha mambo katika jamii kwa haraka zaidi EG SIYAGA