UHURU WA KWELI
Price:
10,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Feb 09, 2021
Product Views:
2,778
Sample
Uhuru wa Kweli katika Kristo Yesu na matokeo ya kazi ya msalaba
Kitabu hiki UHURU WA KWELI ni kitabu kinachomueleza na kumfunua Yesu Kristo kama Mkombozi aliyetusaidia kuwa huru kupitia neema yake aliyoifunua kwa kazi yake ya msalaba. Kazi hiyo inatusaidia kuponywa, kufunguliwa na kuwa na mafanikio kamili. Bwana Yesu alikuja kusuluhisha chanzo cha matatizo yote.Kitabu hiki kitakusaidia kupata ufahamu juu ya mambo yafuatayo:-
- Kumsaidia mtu aliyeathirika na ulevi mbaya (bad addictions) wa aina zote ulioshindikana kupitia neema ya Kristo.
- Kuwa na mtazamo sahihi ambao utapelekea kuwa na imani itakayokusaidia kudhihirisha uponyaji, ustawi (mafanikio) na kuishi maisha ya kimbingu ukiwa duniani kupitia neema ya Kristo.
- Kuwa na ufahamu juu ya kuwa na udhihirisho kamili juu ya huduma, kazi, kipawa na karama zilizoko ndani yako kupitia neema ya Kristo.
- Namna ya kulitimiza kusudi la Mungu kikamilifu kupitia neema ya Kristo.
Kwa Neema ya Roho Mtakatifu nakukaribisha tuweze kujifunza UHURU WA KWELI katika Kristo Yesu ili tuweze kufikia uponyaji, ukombozi na mafanikio kamilifu kama Mungu alivyo kusudia katika maisha yetu.
UMEBARIKIWA