UGONJWA WA KORONA, 666 NA ULIMWENGU MPYA WA KISAYANSI
KITABU HIKI KINAHUSU UKWELI MZITO KUHUSU UGONJWA WA KORONA, 666,CHANJO YA KORONA, ULIMWENGU WA KIDIJITALI NA KUELEKEA ZAMA ZA AKILI BANDIA.
Mambo yanayotokea katika ulimwengu wetu wa
leo hatuna budi kuyafikiria sana kwani kila mahali
ulimwenguni tunaona ghasia na misukosuko
pamoja na milipuko ya magonjwa ya kutisha kama
huu ugonjwa ulioibuka hivi karibuni yaani korona
[uviko 19/covid 19] bahari, maziwa na mito
kuchafuliwa, miti inaangamizwa, mabadiliko
makubwa ya hali ya hewa [climatic change] na
watu maelfu kwa maelfu kukimbia nchi zao ili
kuondokana na hatari, maafa, njaa, vita na vifo.
Si ajabu kwamba watu wale wanaoaminiwa kuwa
manabii waliyatabiri mambo hayo yote kama vile
mtume petro alivyosema ‘’nasi tunalo lile neno la
unabii lililo imara zaidi ambalo mkiliangalia kama
taa ing’aayo mahali penye giza mwafanya vema [2
Peter 1; 19] Edson mkonge mwandishi wa kitabu hiki amezungumzia masuala yahusuyo imani,
kuhusu matukio yanayoendelea hivi sasa
ulimwenguni hasa ugonjwa wa korona na
kuelekea ulimwengu wa kidijitali.
Kile ambacho mungu amesema katika maandiko
matakatifu ya manabii wake, kwani wakati ujao
unatisha na kukatisha tamaa, lakini liko tumaini
Kwa wanaomwamini Mungu na maandiko yake.
Matumaini hayo ya maisha bora, yenye amani na
raha yang’aa mioyoni mwao watakaokisoma
kitabu hiki.