Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Ufunuo Wa Yohana - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali
Best Seller

UFUNUO WA YOHANA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
30,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Mar 11, 2024
Product Views:
694
In category:
Sample

Kitabu cha Ufunuo wa Yohana ni mojawapo ya vitabu muhimu sana ndani ya Biblia, hasa kutokana na sababu ya kuhesabika kuwa ni kitabu kigumu kueleweka, na hivyo kuogopwa kusomwa na watu wengi. Kitabu hiki kinajulikana kuwa ni cha unabii wa agano jipya sawasawa na vitabu vya manabii wa agano la kale. Kinaitwa ni ufunuo kwa sababu maneno yaliyomo ndani yake si ya hekima ya Mungu kupitia \\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\r\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\nmwanadamu kama ilivyo ndani ya vitabu vingine, bali ni maneno na sauti ya Yesu mwenyewe akinena kupitia mtumishi wa Mungu Yohana, huku akimwonyesha funuo mbalimbali na kumwamuru kuandika kila aliloliona na kulisikia, kwa macho na kwa masikio yake.

Kutokana na ufunuo wa Yohana uliomo ndani ya kitabu \r\nhiki, kumetokea mafundisho mengi sana yanayotofautiana na kuzaa imani \r\nnyingi zinazopingana ndani ya madhehebu ya aina moja, wakati mwingine \r\nhata ndani ya chuo kimoja cha theolojia.Tofauti hizi zote zinatokana na \r\nkutofautiana katika njia za kufasiri ufunuo, unabii pamoja na Maandiko \r\nmengine yote. Wengine wanatumia kanuni maalumu zinazowaongoza kupata \r\nmaana, na wengine hufasiri kwa kutumia historia, jiografia,na pengine \r\nkila mtu kudai amepata ufunuo wake binafsi kutoka kwa Mungu. Mambo haya \r\nyote yameendelea kukifanya kitabu hiki kionekane kuwa kigumu sana, na \r\nwengi \\kukiogopa hata kukisoma, wakiamini kuwa ni kitabu kilichojaa siri\r\n za Mungu ambazo ni vigumu kwa mwanadamu wa kawaida kuzielewa. Hata \r\nimekuwa, mtu yeyote nakihubiri kutoka katika kitabu hiki, kunatokea \r\nmambo mawili: kwanza, mhubiri mwenyewe kutokujiamini katika kile \r\nanachohubiri; pili, wasikilizaji kutothamini kile kinachoelezwa kwa \r\nsababu wamejenga dhana potofu ya kuwa kitabu hiki hakuna anayekielewa.


Baada\r\n ya kufundisha kitabu hiki miaka mingi katika semina mbalimbali pamoja \r\nna chuo cha Biblia, nimepata uzoefu mkubwa zaidi kutokana na changamoto \r\nmbalimbali nzinazotokana na maswali mengi wanayoyapata kwa wahubiri wa \r\nInjili wanaohubiri kutoka ndani ya kitabu hiki, lakini hawako tayari \r\nkujibu maswali ya wasikilizaji. Wengine wanakuwa wameshika mafundisho \r\nhayo bila uthibitisho wowote wa maandiko, na hawako tayari kubadili \r\nmtazamo wao hata kama wataona ukweli. Kwangu mimi, kumsikiliza kila mtu \r\nna imani yake na kufuatilia maeneo ambayo ni misingi yake imejengwa \r\nkatika Biblia, imekuwa msaada mkubwa kwangu kuniongoza kukiandika kitabu\r\n hiki ili kuwasaidia wanafunzi wote wa Biblia wanaotaka kujifunza \r\nmaandiko  kwa uthibitisho wa andiko kwa andiko, bila kuingiza mawazo na \r\nfikira za kibinadamu. Kila msomaji sharti ajue kwamba Biblia inaweza \r\nkujitafsiri yenyewe bila kuhitaji msaada wa mawazo ya mtu.


More Products On Discount
5,000 Tsh. 4,499 Tsh.

Sold by: Daudi Lubeleje

30,000 Tsh. 20,000 Tsh.

Sold by: Lackson Tungaraza

10,000 Tsh. 7,000 Tsh.

Sold by: Martin Tindwa

25,000 Tsh. 10,000 Tsh.

Sold by: Msafiri Lwihula

More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

GetValue Recommendations
Old is Gold