UFALME WA MUNGU
Ufalme wa Mungu ni somo ambalo halifahamiki vema na wakristo wengi, pamoja na kwamba, ni somo muhimu kwa kila mkristo kulifahamu vizuri. Injili zinautaja ufalme wa Mungu kwa njia tatu tofauti. (1) Ufalme wa Mungu; (2) Ufalme wa mbinguni; (3) na Ufalme. Wengine wanaamini kuwa, ufalme wa Mungu na ufalme wa mbinguni pamoja na ufalme, ni mambo matatu tofauti.
DIBAJI
Kwa mara nyingine tena namshukuru sana Mungu, kwa neema yake kuniwezesha kutoa kitabu kingine kiitwacho “Ufalme wa Mungu” ambacho ninaamini kabisa kuwa, kitakuwa baraka kwa watu wengi wapendao kujifunza ukweli wa Biblia.
Tangu Mungu aliponipa adhabu kubwa katika miaka ya 1980 kutokana na kufundisha mambo ambayo nilikuwa sijayafanyia utafiti wa kutosha, ingawa nilikuwa natumia elimu yangu ya Theolojia ya Biblia; lakini baada ya miaka kumi ya kutulia miguuni pa Mungu na kutafuta ukweli wa Biblia, mbali na mafunzo yangu ya Theolojia; ndipo Mungu aliniwezesha kupata nuru upya ya kufundisha Biblia kwa kutumia kanuni mbalimbali za kusoma na kufasiri Maandiko matakatifu. Tangu mwaka wa 1993 mpaka sasa, nimeendelea kufundisha masomo mbalimbali yaliyofanyiwa utafiti wa kina na usahihi,kulingana na kanuni mbalimbali za kufasiri Biblia.
Si kwamba niko kinyume na theolojia, la hasha! Nimesoma theolojia, na bado ninaendelea kujifunza theolojia. Masomo ya theolojia ndiyo yaliweza kunifungua fahamu zangu kutoka katika uchanga wangu wa nelimu ya Mungu, hata kufikia ukomavu. Mambo niliyoyagundua mpaka sasa ni kwamba, elimu ya Biblia haiko kama jiwe ambalo hata baada ya miaka mia, utalikuta liko vile vile. Mafundisho mengi katika theolojia ya Biblia yaliandikwa na waalimu maarufu vipindi mbalimbali kwa karne zaidi ya kumi zilizopita. Ukweli ni kwamba kama waandishi hao wangekuwapo leo, naamini kabisa\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\r\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\nkuwa wangekuwa wamefanya masahihisho mengi sana katika mafundisho yao, kwa sababu kuielewa Biblia tunahitaji ufunuo wa Mungu.
Mpaka sasa nimeandika vitabu kadhaa nikijibu maswali tata yanayotokana na masomo mbalimbali ya Theolojia, ambayo hayakubaliani na ukweli wa Biblia. Baadhi ya masomo hayo ni kuhusu “Utatu wa Mungu” Biblia inasemaje kuhusu utatu? Je, Mungu amejifunua kwa njia tatu, au Mungu ana nafsi tatu? Kuhusu “Kitabu cha Ufunuo” Je, kitabu hiki ni Ufunuo au ni Unabii? Mambo yaliyomo ni ya kuyatazamia au yamekwisha kutimia? Je, kuna tofauti kati ya “Kurudi kwa Yesu mara ya pili, na Unyakuo?” Je, dhiki kuu ni kwa ajili ya waovu au kwa ajili ya kanisa? Dalili kuu ya kurudi kwa Yesu ni ipi? Je, ni kweli Mwana hajui siku ya kuja kwake? Mbinguni ni wapi? Je, ni kweli Yesu alikwenda kuandaa mji mbinguni? Na mengine mengi.
Kitabu hiki kinafundisha juu ya somo liitwalo “Ufalme wa Mungu” au “Ufalme wa Mbinguni.” Pia kitabu hiki kinajibu maswali mengi ambayo yamesababisha wakristo wengi kutokukubaliana kwamba, Ufalme wa Mungu uko hapa duniani au uko mbinguni? Je, Yesu anatawala sasa au atatawala katika kipindi cha miaka elfu? Je, miaka elfu ni halisi au ni lugha ya fumbo la kibiblia? Je, kuna usawa kati ya maneno haya; elfu na elfu moja? nJe, Kanisa linatawala sasa pamoja na Kristo au litatawala baadaye? Je, utawala wa Yesu utakuwa ni utawala halisi wa kidunia au ni utawala wa kiroho? Na maswali mengine mengi.
Nakualika mtu wa Mungu uwaye yote yule kufuatana\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\r\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\\nnami katika kukisoma kitabu hiki, ambacho hakifundishi habari za itikadi za dini au dhehebu lolote, bali kinafunua ukweli wa Biblia kwa kutumia kanuni mbalimbali za kufasiri maandiko matakatifu, ili kuthibitisha ukweli jinsi Biblia isemavyo kuhusu somo husika.
Ubarikiwe na Bwana!