UADILIFU WA KIONGOZI
Uadilifu Ni sifa ya msingi na ya lazima kwa Kiongozi.Kiongozi akipoteza uadilifu anapoteza uhalali wa kuingiza na kuaminiwa na wafuasi wake.
Tatizo kubwa lililopo siku za leo sio kukosekana kwa viongozi,bali kukosekana kwa viongozi waadilifu.Hili tatizo ni kubwa hususani katika bara letu la Afrika. Ndani na nje ya kanisa kilio ni kimoja juu ya viongozi waadilifu. Tatizo la kukosekana kwa uadilifu miongoni mwa viongozi ni kubwa katika kizazi cha leo, na ni lazima sauti zipazwe kulizungumza.
Siku za leo kumekua na uhaba wa kupata viongozi waaminifu na wasiobadilika, na watu ambao wanategemewa wanazidi kutoweka.
Leo kuna uaminifu kidogo sana katika jamii inayotuzunguka. Tuko kwenye kizazi ambacho hakitaki kujitoa kuwa na uaminifu katika lolote. Uaminifu ni neno ambalo halisikiki sana katika siku za leo.
Sio neno maarufu tena.Naamini wewe unayesoma kitabu hiki, utapata hamasa ya kuwa kiongozi muadilifu. Na kuamua kusimama na kuwa miongoni mwa
viongozi waadilifu wachache ambao Mungu amejisazia. Haijalishi watu wengi wanakwenda njia ipi. Kitabu hiki kitakusaidia
ubaki kwenye njia kuu ya uadilifu na kuacha njia za mkato.
Kitabu hiki kinamfaa kila aliyeitwa kuwa kiongozi ndani na nje ya kanisa. Kwa kiongozi wa ngazi yoyote ile, kitabu hiki ni hazina bora ya kukujenga na kukuimarisha.