TIMIZA NDOTO YAKO YA KUWA MUHUDUMU WA AFYA
Una ndoto ya kuwa MUHUDUMU WA AFYA? Ungependa kuwa daktari, muuguzi, mtaalamu wa maabara, mfamasia, muhandisi wa vifaa tiba, mtaalamu wa mionzi, afisa lishe..?Pata ufafanuzi na majibu ya maswali yako yote kuhusu taaluma ya afya ili uweze kufanya chaguo sahihi wapi panakufaa.Vilevile utapata kujua nini ufanye ili uweze kufikia ndoto yako, mfano utapata mbinu 10 za kusoma zilizothibitishwa kisayansi, namna ya kupata ada, na mengine mengi.
Tiba bora huanza na wahudumu bora wa afya. Wahudumu bora ni wale wenye karama ya taaluma hii. Mara nyingi watu sahihi wamekata tamaa kutimiza ndoto yao ya kuwa wahudumu wa afya kwa kukosa muongozo sahihi. Kitabu hiki ni muongozo ambao utamulika njia yao ili waweze kufikia lengo. Pengine waliokata tamaa ndio ambao wangegundua tiba za magonjwa sugu! Bila kujali umekutana na changamoto gani amka tena, hujachelewa, pambana jamii inakutegemea na mazuri yanakungoja.
"Together hand in hand we forge foward"