The Garden Of Thoughts
The Garden Of Thoughts
Akili yako ni kiungo hai, kinaweza kukua, kudumaa na hata kufa kabisa ikiwa wewe ungali hai. Tunaishi na vijana wengi wenye miaka kati ya 20 na 40 ambao ni wafu tayari ingawa wengi husubiri mpaka wafikapo miaka 60 mpaka 70 au zaidi ndipo huweza kuzikwa Tuna vijana wengi waliokufa kiakili na wanaishi kwa kutegemea bahati na chochote ambacho maisha yatawaamuria. Vijana wengi wasichokifahamu ni kuwa, ndani ya kila kijana kuna simba imara na mwenye uwezo wa ajabu sana. Lakini kutokushughulishwa kwa akili ya kijana humfanya simba wa ndani yake (uwezo wake wa asili) kusinzia na kumfanya ajione ni paka na si simba tena. Kitabu hiki na mifano yake iliyotumika imelenga kumwamsha Simba aliyelala ndani yako na kukufanya mtu wa thamani na mwenye kufanya yale yaliyoaminika kuwa hayawezekani. Kitabu hiki ni funguo sahihi wa kuufungua mlango wa ukuu wako uliokusudiwa na Mungu.