TEMBEA PAMOJA NA YESU MUNGU
Kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao. 2Wakorintho 6:16.
Mwandishi alipata msukumo wa kuandika kitabu katika Roho Mtakatifu kupitia maono aliyoyaona mnamo mwaka 1989. Mwandishi aliona katika njozi usiku, mwanamke mmoja amezaa mtoto. Yule mwanamke alimkabidhi mtoto huyo kwa mwandishi. Mwandishi alianza kumfundisha mtoto kwa kuimba na kutembea pamoja naye huku amemshika mkono.
Waliimba Tembea na Yesu tembea (pambio ililojulikana sana miaka hiyo ya 80). Baada ya muda, mtoto huyo aliaweza kutembea na kuimba pambio Tembea na Yesu Tembea. Baada ya hapo, Mwandishi alitaka kumkabidhi mtoto huyo kwa mama yake lakini mama yake hakuonekana. Maono yaliishia hapo. Ujumbe huu ni sawa na maandiko yasemayo: Kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 2Kor 6:16.
Mwandishi anaamini kuwa kitabu hiki kina msingi na uvuvio katika Mungu. Ndani yake kuna mafundisho ambayo yatakuwa ni msaada kwa wote wanaotaka kuishi maisha ya utakatifu katika kutembea na Yesu (Mungu) pamoja na wale watakaotamani kuingia katika mkakati huo wa maisha mapya ya kiroho.
Tembea Pamoja Na Yesu Kristo (Mungu)
7
Katika kitabu hiki Tembea pamoja na Yesu (Mungu), utapata fursa ya kuelewa kwa upana jinsi ambavyo Mungu amepanga kukaa na kutembea katika maisha ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo pamoja na Roho wake (Roho Mtakatifu). Katika mada hizo utapata kujua, awali ya yote, juu ya Wokovu, muujiza mkubwa kuliko yote ambao ni muujiza wa Kutembea na Yesu Kristo, na kuishi pamoja naye kama mwokozi wa maisha.
Utapata pia kujifunza juu ya mambo ya muhimu katika kutembea na Mungu (Yesu) ili kuendelea na maisha ya ushindi endelevu katika Wokovu. Aidha, kutembea na Yesu ni kuwa pamoja naye katika ‘njia ile’ ambayo ni njia ya utakatifu, njia ya Uzima, njia ya kwenda kwa Baba. Yoh. 14:6.
Katika njia hiyo kuna dhiki au mapito lakini pia kuna uhakika wa ushindi kwa imani katika Yesu Kristo. Vile vile utajifunza vile ambavyo kutembea na Yesu ni kuwa tayari kutumika katika ufalme wa Mungu hapa duniani, hatimae kukaa na Mungu milele. Hii ni habari njema kwako msomaji wa kitabu hiki, kuitambua fursa ya ajabu iliyopo mbele yako kuhusu KUTEMBEA PAMOJA NA YESU au KWENDA PAMOJA NA MUNGU.
Neema ya Mungu ikuwezeshe tuwe pamoja. Amina.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza