Teka Mafanikio Yako
Teka Mafanikio Yako Wekeza katika kuifanya dunia kuwa bora zaidi ya ulivyoikuta. Tengeneza historia njema katika dunia yetu kwa kuleta mabadiliko chanya duniani.Karibu tujifunze haya kwa pamoja.
Mafanikio pia yanafananishwa na kisima chenye kina kirefu nyikani, kisima chenye maji mengi na safi. Ili kupata maji ya kisima hicho na kuyatumia kwa shughuli zetu za kila siku, kunywesha wanyama wetu na kumwagilia mazao yetu yapate kustawi, hatuna budi kujifunza njia nzuri ya kuyateka maji hayo kutoka katika kisima hicho chenye kina kirefu. Kwenye kitabu hiki tunaenda kujifunza jinsi ya kuyateka maji hayo kwa njia mbalimbali rahisi na kuweza kuyatumia vyema katika kujiletea maendeleo endelevu huko nyikani. Tunaenda kujifunza jinsi ya kutafuta maarifa yanayohitajika nna namna nzuri ya kuyaweka maarifa hayo katika matendo ili yaweze kufanyika kuwa mtego bora wa kuyavutia na kuyanasa mafanikio. Tunaenda kujifunza jinsi ya kuwa na fikra chanya siku zote tunapoendelea na mchakato wa kuteka mafanikio yetu. Kuna siku mitego yetu itakatwa, kuna siku mitego yetu haitanamata kitu, kuna siku mitego yetu itaonekana haifaikitu; ni jambo jema kutambua la kufanya katika mazingira kama hayo. Inawezekana, Timiza Wajibu Wako.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza