TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA
Tatizo ni RasilimaliWatu Tunaowapoteza
Kwa siku nyingi sasa kumekuwepo na
malalamishi kutoka kwa watu mbalimbali, ndani na nje ya bara la la AFRIKA,
malalamishi haya haswa yanaelekezwa kwa wazungu na wakoloni na watu nchi za
nje. Watu wengi wamekuwa wakilalamika kwamba sasa bara la Afrika lingekuwa
limepiga hatua kubwa sana kama wasingekuwa wakoloni waliotawala nchi hizi za
Afrika na kuchukua rasilimali nyingi sana. Katika kitabu hiki utakutana na
mtazamo wa tofauti kutoka kwa mwandishi. Mwandishi atakuonesha kwamba
rasilimali zilizopotea si tatizo kama ambavyo watu wengi wanafikiri. Hii ni
kutokana na ukweli kwamba rasilimali bado zinazidi kupotea mpaka sasa hivi.
Kila mtu ni shuhuda juu ya madini, wanyamapori na mchanga ambao umekuwa ukizidi
kubebwa na kupelekwa nje ya nchi kila mwaka, ingawa wakoloni hawapo.
Si hilo tu bali watanzania na waafrika
kwa ujumla wamezidi kuwa nyuma kwa mambo mengi ikiwemo mambo ya uwekezaji,
uhuru wa kiuchumi, sayansi, utafiti kutaja ila machache.
Hii ni kutokana na imani ya watu wengi
ambao wanaamini kwamba mwekezaji ni mtu kutoka nje ya nchi na wengine wanaamini
kwamba vitu vingine si vya viwango vyao bali vinastahili kufanywa na wazungu.
Basi kwa hali hii bila shaka utakubaliana na mimi kwamba TATIZO SI RASILIMALI
ZILIZOPOTEA.
Sasa kama tatizo si raslimali zilizopotea
tatizo ni nini?
Katika kitabu hiki utapata kujifunza
kwamba rasilimali watu zinazopotea sasa hivi. Kwa sasa tunazipoteza
rasilimaliwatu kwa njia nyingi sana. Hii ni kutokana na watu wengi kutokujua
kwamba wanao uwezo mkubwa sana ndani yao ambao wanapaswa kuutumia ili uwatoe
sifuri mpaka kileleni. Njia hizo zinazosababisha tupoteze rasilimali watu, sasa
zimeelezwa ndani ya kurasa za kiabu hiki.
Vijana sasa wanashinda katika vijiwe vya
zama za taarifa ambayo ni mitandao ya kijamii kama wasapu, instagram,
twitter, na facebook. Vijana wanapoteza muda mwingi kujadili vitu
ambavyo havina manufaa kwao na kwa jamii yetu. Vijana wengi wanaamini kwamba
mtu fulani ambaye yuko sehemu fulani katika nchi fulani ndiye anayehusika na
kufanikiwa kwao. Ndio maana muda mwingi sana unawakuta mtandaoni wakipoteza
muda kwa kujadili vitu ambavyo havina maana. Wanalamikia serikali juu ya ajira.
Lakini vijana hao hao unawakuta wanazurura mtaa mmoja mpaka mwingine.
Wanazurura kutoka kwa mjomba kwenda kwa
shangazi mara kwa bibi, mara kwa babu upande wa mama kizaa mama. Wanazurura kwa
kisingizio cha kwamba hawana ajira au
kisingizio cha ninatafuta ajira.
Lakini hata hivyo wale wanaowapokea nao
wanazidi kusababisha tupoteze rasilimali muhimu ambazo zingeweza kuanzisha
kitu. Rasilimali ambazo zimesubiriwa
zina mziki ndani yao, rasilimali zenye viwanda katika fikra zao.
Kila mtu kazaliwa akiwa mshindi, na kila
mtu ndani yake zimewekwa mbegu za ushindi. Maisha mazuri, utajiri, ushindi,
mahusiano mazuri, amani, kazi nzuri na biashara iliyofanikiwa. Vyote hivi ni
haki ya kuzaliwa ya kila mtu. Lakini kuzaliwa ukiwa mshindi haitoshi. Kama
haupo tayari kulipa gharama ya ushindi. Unapaswa kujua wapo unaenda na kwa nini
unaenda huko.
Kila mara jiulize swalije, mimi……(weka
jina lako) niko wapi? Ninafanya nini? Je, nimekuja hapa kufanya nini? Kama
utajikuta hufanyi kile ambacho unapswa kufanya hata kama wewe umezaliwa
mshindi, my friend, ushindi utausikia redioni. Umezaliwa mshindi lakini
unapaswa kuhakikisha kwamba unalipa gharama ya ushindi na kufanya kazi
kiushindi kila wakati.
Kisome kitabu hiki mwanzo mpaka mwisho maana
kuna mambo mengi sana ya kujifunza.
Hakika usiruke wala kutafuta sura ambazo wewe unaona kama zinakufaa.
Wewe ni mtu wa muhimu sana na jamii nzima imesubiri na inataka kusikia kutoka
kwako. Badili mtazamo wako ili uweze kubadili maisha yako.
Kuna uwezo mkubwa sana ndani yako ambao
bado haujaufahamu na bado haujaanza kuutumia. Kama wewe ni moja ya watu ambao
wangependa kuutumia uwezo huu mkubwa ulio ndani. Kama wewe ni moja ya watu
ambao wangependa kuitumia dhahabu hii kubwa sana ambayo haijachomwa hata
kidogo, basi kitabu hiki kinakufaa sana, kwa hakika umeshikilia hazina
itakayobadili maisha yako. Badili fikra zako kwa kusoma kitabu hiki. Haitoshi
tu wewe kusoma kitabu hiki na kutulia. Hatua
madhubuti zinapaswa kuchukuliwa baada ya wewe kusoma kitabu hiki.
Msimamo wa mwandishi ni ule ya kwamba mtu yeyote anaweza kukuweka katika njia
sahihi, lakini hawezi kukuamrisha wewe kuitembea njia hiyo. Kitabu hiki
kinaonesha njia tu! Ila suala zima la kuifuata njia hiyo lipo juu yako.
Wewe Ni Zaidi Ya Ulivyo Sasa
Chukua hatua sasa
Tukutane kwenye meza ya
wanamafanikio!!!!
Tukutane kwenye mzunguko wa
wanamafanikio!!!
Ndimi,
Godius Rweyongeza
($onga mbele)
Kocha, mjasiliamali na mwandishi
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza