Tathmini Ya Ndoa - Miaka 5 Makosa 50
Jifunze kufanya Tathmini ya Ndoa yako kila wakati
Wengi wetu tumezaliwa katika ndoa au wengine pia hatukupatikana ndani ya ndoa. Kwa vyovyote vile tayari tupo hapa duniani. Ndoa ni taasisi nyeti sana ambayo inapaswa kueleweka vizuri na wanandoa na hata wasio ndani ya ndoa.
Nyakati hizi tumeshuhudia ndoa nyingi zikigubikwa na migogoro ambayo imepelekea watu kuachana, watoto kukosa uangalizi na hata vitendo vya kikatili dhidi ya wanandoa.
Lakini tunapaswa kufahamu ya kuwa ndoa ni taasisi aliyoianzisha Mungu mwenyewe, na kuweza kufahamu namna bora ya kukaa ndani ya taasisi hii ni kujifunza kile neno la Mungu linasema kuhusu ndoa.
Kila zama zina changamoto zake, hivyo hata ndoa katika karne hii ya 21 ina changamoto zake. Waandishi Isaack na Maria walio katika ndoa tangu 2012 wanashirikisha Makosa 50 ndani ya miaka 5 ya awali ya Ndoa yao na namna Hekima ya Mungu katika neno lake inavyowasaidia kuzitatua changamoto hizo.
Kitabu hiki ni mahsusi kwa wanaotarajia kufunga ndoa, wanandoa wachanga na hata wazoefu, wakufunzi wa masuala ya kijamii na kila mmoja wetu mwenye nia ya kufahamu hekima ya Kimungu kwenye masuala ya Kiroho, Kiutawala, Kiuchumi, Kazi, Mahusiano na Afya ndani ya Ndoa.
Namna bora ya kuifanya ndoa yako kuendelea kuimarika kila siku ni kukubali kuwa Mwanafunzi wa maisha ya ndoa.
Nunua nakala yako sana na ujifunze juu ya makosa 50 ambayo unaweza kuwa umefanya au ukaepuka kuyafanya katika maisha yako ya ndoa.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza