Tasnia Ya Muziki Mkombozi Wa Vijana
Kitabu hiki kimelenga hasa kutangaza yale yaliyopatikana katika utafiti. Ni nini kinafanya wasanii wa Bongo Flava hapa Dar es Salaam wachume kipato duni? Hata hivyo kwa mtazamo mpana kinalenga kuangalia kazi zenye staha kwa watu wote na zaidi kwa vijana; kundi la watu wenye nguvu na nafasi kubwa ya kujenga jamii. \r\n\r\nWashiriki katika utafiti walikuwa wasanii maarufu na wasio maarufu, vituo vya redio, vituo vya kuandaa muziki, wauza kazi za muziki, washiriki toka BASATA, COSOTA, ILO –Dar es Salaam, Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Chuo cha kung’arisha vipaji. Taarifa zilipatikana kupitia madodoso, usaili wa ana kwa ana, na nyaraka mbalimbali za mambo ya vijana.\r\n\r\nUtafiti uligundua kuwa wasanii wa Bongo Flava hupata kipato chao kupitia tamasha mbalimbali za muziki, mauzo ya kazi zao za kisanii na shughuli anuwani ziwahusishazo vijana hao. Utafiti ulithibitisha kuwa wasanii wa Bongo Flava hawakupata kipato sahihi kulingana na juhudi zao. Ilibainika kuwa kipato kidogo husababishwa na kazi zao duni, usimamizi dhaifu wa shughuli zao na kukosekana kwa mwongozo sahihi toka katika uongozi wa tasnia ya muziki. Matokeo zaidi ya utafiti yalionyesha kuwa bila kuwanyanyua wasanii hawa itakuwa vigumu kuifanya Bongo Flava kuwa ajira yenye staha.\r\n\r\nAidha uchunguzi uligundua kuwa Bongo Flava huzalisha nafasi za ajira kwa wasichana na wavulana. Hata hivyo kuna haja ya kuimarisha elimu ya muziki, mafunzo endelevu kuimarisha umoja wa wasanii ili uweze kutetea maslahi yao na hivyo kuifanya kazi hii kuwa ile yenye staha.
Ukosefu\r\nwa ajira ni moja ya matatizo makubwa katika nchi mbalimbali duniani kote;\r\nzilizoendelea na zinazoendelea kukua kiuchumi. Tatizo hili hugusa watu wa rika\r\nzote, wazee kwa vijana, lakini vijana huguswa na kuathirika kupindukia.
Kuna\r\nsababu anuwai za ukosefu wa ajira kwa vijana; ukosefu wa ujuzi takikana, ukuaji\r\nmdogo na dhaifu wa uchumi, kukua kasi kwa idadi ya vijana na kadhalika.
\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n
Vijana\r\nnchini Tanzania, hususani mijini, wanatumikisha vipaji vyao kujipatia ajira.\r\nTasnia ya burudani na muziki inawapokea vijana wengi wa kike na kiume walio\r\ntayari kujituma. Pamoja na juhudi hizo za vijana, ushahidi unaonyesha kuwa\r\nvijana hawa hawanufaiki kiuchumi ipasavyo. Je, sababu hasa za kukosa haki zao\r\nni nini na nini mustakabali wa vijana na vipawa vyao? Maswali hayo na mengine\r\nzaidi yanajibiwa ndani ya kitabu hiki