TAMBUA NYAKATI ZA MWISHO
Ni kitabu kinachoeleza mambo ya nyakati za mwisho kutokana na shuhuda mbalimbali za manabii wa uongo.
TANGULIZI
Napenda kukusalimu ndugu msomaji katika Jina la Yesu Kristo na Amani iwe pamoja nawe.
Kitabu hiki kinaitwa “TAMBUA NYAKATI ZA MWISHO”. Ni Kitabu ambacho kinafungua macho watu kuhusiana na mambo ya nyakati tulizopo kwa sasa. Ili tuwe makini tusidanaganyike tukapotea katika kweli ya Mungu. Kitabu hiki ukikisoma kinakupa nguvu ya Kiroho na kufungua Ufahamu katika mambo ya Kiroho, kinakupa pia ujasiri wa kusimama na kumtafuta Mungu kwa kusoma Neno lake na kufuata amri zake.Kitabu hiki kimesheheni mambo mbalimbali yatokanayo na vitu nilivyokutana navyo katika huduma za kiroho. Mahali nilipotegemea faraja nilijikuta nakutana na kuumizwa, kukatishwa tamaa, kudharaulika na baadhi ya watu walio katika ngazi za juu kiutumishi.Kwa hali ya kawaida huwezi kufikiria kuwa hayo yanaweza kutokea katika NYAKATI HIZI ZA MWISHO. Lakini haya ni mambo yapo na yanatoke katika nyakati hizi tulizo nazo, hivo nakusihi mpendwa msomaji wa kitabu hiki haya ninayokwenda kukushirikisha ni halisi na nimeyapitia. Baadhi ya watumishi hujihusisha na tamaa ya fedha, uzinzi, mafundisho na imani potofu, unabii wa uongo, uchawi {kuwatawala watu kwa maneno}. Hivi ni vitu nimevishuhudia mimi mwenyewe sio vya kusimuliwa.
Mpendwa msomaji inawezekana uliumizwa au kukatishwa tamaa katika mambo ya kiroho au katika huduma yako au kwa kipawa chako usihofu samehee na mwamini Mungu simama tena. Mungu humrudia yule wake’ amini nakwambia hata kuacha atakusimamisha tena na atakukumbusha hata katika kuanguka kwako.Binadamu hubadilika lakini Mungu habadiliki kamwe ndio maana Mungu hutupa nafasi nyingine ya kusimama tena.Wapo watu walioumizwa sana na mwisho wake wamekata tamaa ila ni jambo moja yatupasa kujua hao ni binadamu tu na sio Mungu. Tambua Mungu yupo kwa ajili ya kuponya nafsi na moyo wako nawe ukasimama tena.
Mpendwa msomaji endelea kusoma kitabu hiki na Mungu akubariki pia.
ISAYA 45:3Nami nitakupa hazina za gizani na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israel.
Mungu akutie nguvu unapoendelea kusoma kitabu hiki.
Amina!!!!!!
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza