Tabia Za Watu Walio Fanikiwa
Badiri Fikra Zako Badiri Maisha Yako
Tabia ya mtu hutokana na kujirudia kwa shughuli anazozifanya kila siku hivyo huamua matumizi yake ya muda kwa kumuwezesha kufanikiwa au kutokufanikiwa.Watu wote wenye mafanikio duniani wanatabia zenye kufanana ndiyo sababu kitabu hichi kimekusudia kukuletea elimu ambayo kama utaifanyia kazi utakuwa mtu usiyeweza kuzuilika katika kutimiza malengo yako. Katika kitu pekee cha zawadi ambacho ni mtaji kwa kila binadamu amepewa ni muda na akili.Hivyo kama binadamu akivitumia vizuri vitu hivi viwili anakuwa mtu asiyezuilika katika malengo yake.Kwanza kwenye muda ndiyo mafanikio ya watu wengi yamejikita huko kama mtu atafanya jambo ambalo lilimpotezea muda mwaka uliyopita na akiendelea kulifanya atapoteza miaka yake yote na kupoteza muda maana yake kupoteza maisha.............!