SIRI YA MAFANIKIO YA ELIMU YA MSINGI KATIKA JIJI LA ARUSHA
Siri ya Mafanikio ya Elimu ya Msingi katika Jiji la Arusha Mwaka 2015-2020 ni kitabu kinachoeleza siri 21 zisizosemwa zinazochochea ubora wa ufaulu kitaifa Mtihani wa Darasa la Saba na Upimaji wa Darasa la Nne 2018-2020. Kitabu hiki ni hazina ya kutambua shule bora za msingi katika Jiji la Arusha. Aidha, kitabu hiki kinakufungulia milango ya kutitambua Jiji la Arusha.
Mwandishi wa Kitabu hiki ni Mwalimu Hassan A. Hassani ambaye mtaalamu\\r\\nwa elimu. Alizaliwa katika Mkoa wa Lindi, nje kidogo ya Manispaa ya Lindi. Mwandishi mwaka 2008 alijiunga na masomo ya Shahada ya awali ya Sanaa na Ualimu katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kuhitimu mwaka 2011. Hata hivyo, mnamo mwaka 2012 Mwandishi alijiunga na Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa masomo ya\\r\\nShahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na kuhitimu mwaka 2014.
Mpaka kitabu hiki kinachapishwa Mwandishi ni Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu katika Halmashauri ya Jiji la Arusha. Hiki ni kitabu cha pili kukiandika ambapo kitabu chake cha kwanza ni riwaya iitwayo “Kwaheri” ambayo imeidhinishwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuwa kitabu cha ziada kwa wanafunzi wa sekondari nchini Tanzania.
Ukiniuliza umeifanyia nini dunia? Nitakujibu nimechonga kalamu yangu,\\r\\nnimeiandikia historia Halmashauri ya Jiji la Arusha, historia ya taaluma. Natambua bayana ya kwamba binadamu ni mwanafunzi katika historia ya maisha yake\\r\\nyote. Binadamu hukoma kujifunza mara anapokikabili kifo na kutii.
Lengo la kitabu hiki ni kuhifadhi historia adhimu ya jiji hili kufuatia mafanikio makubwa ya kielimu yaliyopatikana kwa mwaka 2018 na 2020 ambapo Halmashauri hii iliongoza kitaifa kwa Ubora wa ufaulu katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) na Upimaji Wa Kitaifa Wa Darasa La Nne (SFNA). Sambamba na hilo kuwatia moyo mashujaa walioifikisha kileleni halmashauri, kilele cha taaluma. Kwa hakika aonaye baridi ndiye hufuata moto. Arusha Jiji kuna moto, moto wa taaluma, karibu ujifunze.