SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA: DUKA LA REJAREJA
SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA, DUKA LA REJAREJA; Ingawa duka ndiyo limebeba jina la kitabu, siyo kwamba kinaeleza tu kila kitu kuihusu biashara ya Duka hapana, bali ni kila biashara ya rejareja kubwa na ndogo.
Ni biashara inayofanywa na watu wengi zaidi mijini na hata vijijini, zaidi ya asilimia 75% ya biashara zote jijini Dar es salaam ni biashara za rejareja hasa maduka.
Uanzishaji wake ni rahisi usiohitaji mtaji mkubwa, ni kimbilio la walio wengi lakini Je, ili ufanikiwe unazijua mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia? Ungana na mtunzi wa kitabu hiki kujua siri walizopitia wale unaowaona wakimiliki maduka makubwa ya rejareja mjini na kwingineko kote.
Utapata pia fursa ya Kufahamu njia rahisi sana na mifumo ya kudhibiti stoku na hesabu zako kuzuia mfanyakazi au msaidizi wako asikuibie wala kufanya hujuma yeyote faida na mtaji vikabakia vilevile mpaka siku ya kupiga mahesabu.
Njia na mifumo hiyo siyo lazima utumie kompyuta hapana, hata daftari la kawaida tu na kalamu vinatosha.
Mwandishi anakupa uzoefu wake binafsi wa biashara hii ndani ya kitabu kwa picha za rangi alizopiga hatua mbalimbali toka anaanza moja biashara yake Kariakoo mpaka anaajiri mfanyakazi.
Utayafahamu mambo mengi ya kushangaza kuhusu haya maduka ya rejareja kuanzia chumaulete, mbinu za kuvutia wateja za kienyeji na hata zile za kisayansi.
Hatujasahau pia kuonyesha fursa kubwa inayoletwa na teknolojia mpya ya Akili bandia (Artificial Intelligence AI). Jinsi inavyoweza kuleta mapinduzi makubwa katika biashara ya rejareja kwa kuboresha ufanisi na kuokoa muda.
Pia tumeonyesha ni changamoto zipi na hatari teknolojia hii inaweza kuambatana nayo. Siyo kitabu cha kukosa kabisa ikiwa unafanya biashara ya rejareja katika karne hii ya 21.