Siri Iliyo Jificha Kwenye Mafanikio
Siri Iliyo jificha Kwenye Mafanikio
Kushika kitabu hiki mikononi mwako, yaweza kuwa ndiyo bahati kubwa maishani mwako. Yapo mengi (mazuri) utakayojifunza katika kitabu hiki. Watu wengi wanafanya kazi kwa bidii wakitafuta mafanikio. Wanakesha wakipigania ndoto zao, na kufanya kila linalohitajika. Wapo tayari kwa lolote, lakini wanashangaa maisha yao kuendelea kuwa magumu. Wanabaki wakijiuliza maswali mengi kama vile, “Hivi hawa wanaofanikiwa wanafanyaje?”, “Kama bidii ninayo, nakosea wapi?” Na wengine huenda mbali Zaidi na kuanza kufikiria kwamba, “Mtu hawezi kufanikiwa bila kuwa mchawi, mwenye roho mbaya, au kubarikiwa na Mungu.”
Ili kujua siri iliyojificha kwenye mafanikio Endelea kusoma kitabu chako……..!