SIRI 20 ZA USHINDI
Badilisha Fikra Zako Badilisha Maisha Yako.
Kwenye maisha ili uweze kufanikiwa unahitaji kubadilisha fikra zako ili kufikia mafanikio unayohitaji. Siri ambazo nimeandika katika kitabu hiki, nimeandika kwa umakini mkubwa baada ya utafiti wa kina. Siri hizi za ushindi zimeelezwa kwa lugha rahisi na mifano mbalimbali iliyoambatana na nukuu zenye kuleta hamasa. Bila shaka, katika shule zetu hakuna somo ambalo limejaribu kukuelekeza namna ya kupata mafanikio lakini haina maana kwamba uyapuuze yale unayofundishwa shuleni au chuoni. Katika kitabu hiki utajifunza siri ambazo zitakufikisha mbali katika kuyafikia mafanikio unayoyatamani hivyo ni muhimu kuyazingatia yaliyoandikwa humu kwa vitendo.