Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Silaha Za Vita Vyetu - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

SILAHA ZA VITA VYETU

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Aug 26, 2024
Product Views:
32
In category:
Sample

Moja kati ya jambo ambalo huwezi kulikwepa katika maisha yako wewe kama mkristo ni kupigana vita. Biblia inasema katika kitabu cha; Mathayo 10:16 “Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.” Neno hili ni uthibitisho wa kuwa sisi tumezingirwa na adui pande zote za maisha yetu. Kwenye huduma na utumishi wako utakutana na adui wanaokusubiri kukumaliza, kwenye ndoa utakutana na adui ambao wana kazi moja tu ya kuhakikisha ndoa yako inaharibika, katika biashara nako wapo adui wengi ambao wamejiandaa kukupiga. Kwahiyo Mwanangu nenda kauchukue ushindi wako Kwa jina la Yesu.

Kitabu hiki cha “SILAHA ZA VITA VYETU” ni kitabu ambacho kimelenga kumfundisha na kumpa maarifa na hekima mkristo juu ya silaha za kutumia nyakati ambapo atakutana na vita au mashambulizi kutoka kwa adui shetani au adui wanaotuzunguka katika maisha yetu.

Maisha yetu yamezungukwa na maadui pande zote na hii ni kwa watu wote iwe ameokoka au hajaokoka, iwe anamjua Mungu au hamjui Mungu. Maadamu wewe ni binadamu uliyeumbwa na Mungu, utakutana na vita tu. Katika biashara utakutana na vita vyake, katika mahusiano na ndoa utakutana na vita vyake, katika elimu na kazi utakutana na vita vyake, katika siasa nako utakutana na vita vyake na hata katika utumishi na huduma nako utakutana na vita vyake. Kwa hiyo, kiufupi kabisa ni kuwa hakuna eneo lolote utakalokuwepo katika maisha yako ambapo hutokutana na vita.

Sasa ili uwe mshindi katika hilo eneo ni lazima uwe na ufahamu juu ya;

  • Vita unayopigana (Ni lazima ujue sababu nyuma ya vita unayopigwa, hii itakusaidia sana katika kupigana vita vyako kwa akili na ufahamu.)
  • Silaha anazotumia adui kupigana na wewe (Ni lazima pia uwe na ufahamu wa kutosha juu ya silaha na njia ambazo adui anatumia ili kupigana vita na wewe, ukijua silaha za adui na wewe utajua kwa wakati huu utumie silaha gani ili kumshinda.)
  • Silaha gani utumie na kwa wakati upi ili umshinde adui yako (Wewe pia unatakiwa ujue ni silaha zipi utatumia ili kuweza kupigana na kumshinda adui yako).

Haya ni mambo ya msingi ambayo unatakiwa uyazingatie ili kuweza kushinda vita zote ambazo utakutana nazo katika maisha yako.

Hiki kitabu ni kitabu ambacho ndani yake utajifunza juu ya vita na ni kwanini unapigwa vita lakini utajifunza juu ya aina za vita ambazo utakutana nazo katika maisha yako na silaha za kutumia ambazo zitakuwezesha kupigana vita na kushinda.

Mwisho kabisa nimekuwekea muongozo wa maombi ya vita ambayo yatakusaidia kukuongoza kuomba hata kwako wewe ambaye umeokoka hivi karibuni na bado hujui kuomba vizuri. Kwa kutumia maombi hayo utaweza kuomba na kuamrisha adui aachilie milki zako na vyote vilivyo vyako kwa jina la Yesu.

Zaidi ya yote kitabu hiki kitakuwa msaada wako wa karibu siku zote ambapo utakuwa unakutana na vita. Kila mara utakapokuwa unakutana na vita hakikisha unachukua kitabu hiki na kufanya maombi yaliyomo humu na utaona namna ambavyo yatakuletea matokeo.

Neno la Mungu linasema katika kitabu cha;

Yeremia 51:20

“Wewe ni rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunjavunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme.”

Kwa hiyo usiogope kupigana vita mwanangu maana Mungu mwenyewe ataingia vitani na wewe na kukusaidia kushinda vita zote kwa jina la Yesu.

More Products On Discount
5,000 Tsh. 2,500 Tsh.

Sold by: Joyce Mwakajonga

5,000 Tsh. 1,000 Tsh.

Sold by: RAMV MRUMA

25,000 Tsh. 10,000 Tsh.

Sold by: Msafiri Lwihula

98,000 Tsh. 60,000 Tsh.

Sold by: Prophet Pd John

3,999 Tsh. 1,999 Tsh.

Sold by: Daudi Lubeleje

More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
Old is Gold