Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Signs And Tokens - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

SIGNS AND TOKENS

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Aug 29, 2024
Product Views:
22
In category:
Sample

SIGNS AND TOKENS

Ili Imani ya mtu ifanye kazi na imletee matokeo makubwa sawasawa na anavyoamini ni lazima ajifunze kuambatanisha Imani yake na matendo. Neno la Mungu linasema katika kitabu cha; Yakobo 2:14-18 \\\"Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! lle imani yaweza kumwokoa? Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini? Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.\\\"Imani ya mtu yeyote ile ni bure kama haikuambatanishwa na matendo. Kitabu hiki nimekiandika mahususi kwa kuwasaidia watoto wa Mungu kuambatanisha Imani zao na matendo ili waone na kupata matokeo wanayoyatarajia. Humu utajifunza namna ya kutumia vitu mbalimbali vilivyoumbwa na Mungu mwenyewe katika kufanya matendo ya kiimani. Kama Elisha alitumia chumvi hata sisi tunaweza kutumia chumvi, Kama Yesu alitumia udongo na mate hata sisi pia tunaweza kutumia udongo, Kama Musa alitumia fimbo hata sisi tunao uwezo wa kutumia chochote na kuamrisha chochote kututumikia.Kila token iliyoandikwa kwenye kitabu hiki ina uwezo wa kukuletea matokeo makubwa ukifanya kwa ufahamu na kwa Imani. Kupitia hizi token, wapo watakaopandishwa vyeo, wapo ambao watapata watoto, wapo ambao watafunguliwa magonjwa na vifungo mbalimbali. Ni maombi yangu kuwa, token yeyote utakayoifanya sawa na unavyoamini Mungu akutendee hayo.

Katika Biblia tunaziona na kuzisoma habari za manabii, mitume na watumishi mbalimbali wa Mungu na moja ya kitu kikubwa kilichotawala katika kipindi hiko ni ishara na vitendo vya Kiimani ambavyo katika hivyo jina la Mungu lilitukuzwa sana.

Ishara na vitendo vya imani vilivyofanyika ilikuwa ni njia mojawapo ya kumtambulisha Mungu ndani ya maisha ya mtu.
Namaanisha, kutokana na zile ishara na matendo ya imani yaliyofanyika watu waliweza kumjua Mungu na kuamini uwepo wake.

Kila kitendo cha imani kilichofanyika kilipelekea Mungu kusifiwa na kujulikana na wale wasiokuwa wamemjua au kumuamini.

Tuangalie mifano michache ya watu wa Mungu katika Biblia ambao walifanya vitendo vya kiimani na ishara ambazo zilifanya Mungu atukuzwe na kuogopwa na wao kufanikiwa.

 Eliya (Aliizuia Mvua kunyesha na Manabii wa Baali)

Tunaona habari ya Eliya na namna ambavyo alizuia mvua kunyesha isipokuwa kwa neno lake katika kitabu cha 1 Wafalme 17:1-2

Hakuna mtu anayeweza kuamuru mvua kutokunyesha isipokuwa ana nguvu au mamlaka ya kufanya hivyo au amepewa nguvu na mamlaka ya kufanya hivyo na Mungu mwenyewe.

Joshua (Alisimamisha Jua)

Tunasoma katika kitabu cha; Joshua 10:12-15

Kama Joshua alipewa kibali cha kusimamisha jua na mwezi hata wakashinda vita zao hata sisi tukiomba Mungu anaweza kutupa nguvu juu ya vitu na tukavitiisha na vikatutii na sisi tukapata ushindi wetu.

Musa (Alitumia fimbo kufanya ishara na maajabu)
Musa aliitumia fimbo yake kutenda ishara na maajabu lakini pia kufanya kitendo cha kiimani cha kutumia fimbo kugawanya bahari ya shamu na hata wanaisraeli wakapita.
Fimbo ileile iliweza kugeuka kuwa nyoka, fimbo ileile iliyapiga maji na ikafanya yageuke kuwa damu, na fimbo ileile ndiyo iliyoigawanya bahari ya shamu.
Hii inaonyesha kuwa; kama Mungu alitumia fimbo kuwapa ushindi wanaisraeli hata Farao akawaachia, anaweza kutumia na udongo, anaweza kutumia na maji na vyote vilivyomo duniani sawasawa na vile apendavyo.

Elisha (Alitumia chumvi kuiponya nchi)
Tunasoma katika kitabu cha; 1 Wafalme 2:19-22
Kwanini Elisha alitumia chumvi kuyaponya maji ya mji ule?
Ni nani alimwambia Elisha anaweza kuiongelesha chumvi na kuiambatanisha na maneno na ikafanya kitu kilekile alichokiamuru?

Hii ni ishara ya kuwa Mungu ametupa uwezo wa kutumia chochote kilichopo duniani kwa ajili ya manufaa yetu na wengine.
Yesu (Alitumia mate na matope kumponya mgonjwa wa upofu)

Mfano mwingine mzuri ni kutoka kwa Yesu mwenyewe. Tunaona katika Biblia wapo vipofu ambao aliwagusa tu wakapona, wako ambao waliombewa na Yesu na wakapona lakini kuna mmoja ambaye Yesu alitumia mate na udongo na kisha kutengeneza tope na kumpaka kipofu machoni naye akapata kuona tena.

Tunasoma katika kitabu cha: Yohana 9:1-9

Sasa kwanini Yesu alitumia udongo na mate? Hakuna ajuaye ila inaonyesha ya kuwa unaweza ukatumia chochote ambacho ni uumbaji wa Mungu kukuletea matokeo katika maisha yako.

Ukisoma zaidi katika Biblia utakutana na historia nyingi zaidi za watu wa Mungu na namna ambavyo wao walitumia vitu na kuvitiisha na kuwatumikia wao.

Nimeandika hizi chache ili kukuonyesha kuwa haya unayoenda kuyasoma na kuyafanya sio mambo mapya na wala sio vitu vipya duniani.

Hata watumishi wa zamani walitumia chumvi, walitumia mafuta, wako waliotumia mawe nk. kulingana na mafunuo waliyoyapata kwahiyo utakapokutana na vitendo vya imani vinavyokutaka utumie karatasi au chumvi au udongo usione ni kama kitu kipya bali ufanye kwa imani na uone namna ambavyo vitakuletea matokeo katika maisha yako.

More Products On Discount
6,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

3,999 Tsh. 1,999 Tsh.

Sold by: Daudi Lubeleje

5,000 Tsh. 1,000 Tsh.

Sold by: RAMV MRUMA

5,000 Tsh. 2,500 Tsh.

Sold by: Joyce Mwakajonga

7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
Old is Gold