SAYANSI & SANAA YA UPISHI WA CHAPATI LAINI
Sayansi na Sanaa ya Upishi wa Chapati Laini ni kitabu kinachotoa suluhisho la moja kwa moja kwa mtu yeyote anayehangaika kufahamu mbinu za upishi wa chapati laini na tamu. Kina course nyingine pia za mbinu za kuifanya biashara ya supu ikulipe vizuri pamoja na jinsi ya kuandaa mpango wa biashara ya Cafe ya chapati, supu na mchanganyiko wa vyakula vingine.
Ikiwa wewe ni mpishi wa chapati, una cafe ya chakula au tu ungependa kufahamu chapati laini zinavyotengenezwa kitabu hiki kitakusaidia sana.
Na siyo lazima uwe unafanya biashara hapana, chapati ni chakula kinachopendwa sana majumbani na siku yeyote baba au mama unaweza kuamua kuwapikia wanao mlo wa chapati waka ‘enjoy’ kwa mchuzi wa nyama, maharage, maziwa au hata chai.