SAUTI YA YAKOBO MIKONO YA ESAU
JILINDENI NA CHACHU YA MAFARISAYO, AMBAYO NI UNAFIKI
SHILEMBE
Hadithi hii niliipata\\r\\nkutoka kwa Mwimbaji wa nyimbo za Injili anaitwa ANNOINT AMANI anasema…
Namkumbuka Shilembe,\\r\\nRafiki yangu Shilembe. Alikuwa kwenye kampuni ya usafi, alishinda tuzo nyingi\\r\\nkwenye kampuni ya usafi. Siku moja bosi wake alimwambia Shilembe, Jiandae kuna\\r\\nshindano kubwa ni shindano la dunia nzima, tunaaka uchukue tuzo ya usafi wa\\r\\ndunia…Ujulikane dunia nzima Shilembe. Lakini shindano ni gumu Shilembe,\\r\\nlinataka maandalizi makubwa Shilembe.
Shilembe alijisifu\\r\\nsana kwa bosi wake…Nimeshnda tuzo nyingi na huko nako kwa hakika nitashinda.\\r\\nSiku ya shindano ilipofika, Shilembe hakujali…alifua sana nguo zake, zilikuwa\\r\\nsafi. Maana shindano ni la wasafi, lazima awe safi.
Bosi wake\\r\\nalimnong’oneza Shilembe, usije niangusha Shilembe…maana mkaguzi anatoka mbali.\\r\\nMkaguzi huyu si kama wale tulio wazoea Shilembe, nimealika watu wengi nikiamini\\r\\nunashinda Shilembe.
Shilembe alicheka\\r\\nsana, akamwambia Bosi wake, usijali nitashinda tu. Ushindi ni wangu siku zote\\r\\nBosi. Maana nina tuzo nyingi za usafi. Wote wananijua mimi ni bigwa na kila\\r\\nkitu.
Mkaguzi alipofika\\r\\naliwasifu sana washindani, mumependeza sana washindani. Mumenifurahisha sana\\r\\nwashindani. Sikujua kama mtapendeza hivi…HONGERENI. Shilembe akiamini anabeba\\r\\ntuzo.
Mkaguzi akasema\\r\\nshindano la leo, HATUTAANGALIA NGUO ZA NJE, mtakwenda kuvua nguo zote,\\r\\nTUTAWAKAGUA NGUO ZA NDANI.
Aah! Shilembe\\r\\nalishituka, Shilembe aliogopa. Alifua nguo zote, akasahau ya ndani…hakutegemea\\r\\nshindano lile watakagua nguo za ndani. Aibu kwa Shilembe, mtu aliyeshinda sana.\\r\\nAibu kwa waandishi wa habari. Aibu kwa mtu aliyetegemewa ushindi. Alikuwa\\r\\nakifua nguo za nje anasahau za ndani.
Kanisa la sasa wengi\\r\\nwana tabia hii ya SHILEMBE, ni hatari sana. Shetani kawaruhusu watu kuokolewa\\r\\nlakini anawapoteza wakiwa ndani ya wokovu kwa kuwapa roho ya UNAFIKI. Na hapa ndipo lile andiko Yesu alilosema linapata\\r\\nkutimia…
Kwa maana WAITWAO NI WENGI, bali WATEULE NI WACHACHE.
Mathayo 22:14
Andiko la Mwanzo\\r\\n27:22-23, hili ndilo linabeba uhalisia wa kanisa la sasa. Ni jambo ambalo kwa\\r\\nhakika linasikitisha. Ndipo niliposukumwa kwa mzigo na Roho Mtakatifu kuandika kitabu\\r\\nhiki kwaajili ya kanisa la kipindi cha sasa. Kanisa limekubwa na dhambi hii na\\r\\nlimefungwa macho wasielewe kabisa, wanaishi na kuendelea kwenye hali hiyo na\\r\\nkupotelea humo.
Yakobo alikuwa anaenda\\r\\nkwa baba yake Isaka kutaka Baraka lakini akijua kabisa kuwa kwa namna\\r\\nalivyofanya hakustahili, ni dhambi ambayo wengi wa wanaokuona nje HAWATAMBUI\\r\\nkuwa unayo. UNAFIKI NI CHUNGU CHA DHAMBI\\r\\nNYINGINE NYINGI ZA SIRI.
Kitabu hiki kinahusu\\r\\nugonjwa na dhambi mbaya iliyopo kwenye kanisa inayoitwa UNAFIKI, lengo la kuandika\\r\\nkitabu hiki ni kusaidia kanisa na kulifungua macho ili kuondokana na dhambi hii\\r\\nna kuweza kushinda.
Yakobo maana yake ni\\r\\nmtu mdanganyifu na anayetumia udhaifu wa mwingine kujifaisha mwenyewe. Kanisa\\r\\nnalo linatabia hii ya Yakobo.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza