Sanaa Ya Uneni
Sanaa Ya Uneni
Hii ndiyo stadi pekee ambayo hutakiwi kuikosa duniani. Kwenye maisha stadi ya kuzungumza lazima uitafute mwenyewe kwa kulipia gharama ya muda na pesa ili kukuza uwezo wako wa kutambulika, kukuza fani yako, kuimarisha fani yako, uongozi ama biashara/huduma yako. Mamilioni ya watu wamepoteza fursa nono na nyeti kwa sababu wao wanaona ni bora wafe kuliko kuambiwa wasimame mbele kuzungumza chochote mbele ya kadamnasi. Kuwa mahiri wa kuzungumza kunakurahisishia kupanda cheo hata hapo ulipo, kunarahisisha kupata kipato kilichonona kwa kuendesha sherehe mbalimbali, ni rahisi kukubalika na kutambulika, inakupa heshima, kipendwa na jamii kubwa, kuthaminiwa, kusaidìwa na hata kukuza mauzo ya biashara/huduma yako. Umejinyima Mafanikio kwa muda mrefu sana na hii ndiyo tiba rahisi. Amua leo ukisome kitabu hiki na ujilaumu kwanini hukukiona miaka kadhaa nyuma.