SAMEHE TU
SAMEHE TU
Rosaria Materu binti mrembo, msomi na mcha Mungu anajikuta kwenye wakati mgumu baada ya mahusiano yake na kijana makini mhandisi wa mambo ya mawasiliano Deogratias Malisa almaarufu kama Deo Konki kuvurugika. Kitendo cha kuachwa kinamuingiza kwenye hatua ya kuona hakuna maana ya maisha katika kiwango ambacho dunia yake inasimama huku juhudi za kila maneno ya kufariji na kutia moyo toka kwa ndugu, jamaa, marafiki na wataalam wa saikolojia zinagonga mwamba. Lakini anakutana na mafundisho sahihi kuhusu msamaha na kwa nini wakati mwingine ni sahihi kuachwa kitu ambacho kinamponya na kumrejesha katika hali nzuri na kuendelea na maisha ya furaha baada ya kusamehe.
Nikukaribishe uendelee kutiririka na simulizi hii iliyojaa visa, mikasa na mafunzo kwa undani wake na hakika hutabaki kama ulivyo.