Saikolojia Ya Mwanamke
Saikolojia Ya Mwanamke
Hembu fikiria umetoka kupambana kutafuta Hela, kutafuta Maokoto kwa kazi ngumu za kukutoa mwili jasho. Umetoka Ofisini Au Kazini kama umeajiriwa, umetukanwa sana na Bosi wako kazini... ...njiani unakutana unatukanwa, Watu na msala wengine hawakuamini na kukuheshimu kabisa. Ila kila ukiwaza kurudi nyumbani Akili na viungo vyote vinakataa kabisa. Unaona ni bora uende kwenye banda la mpira ukaangalie simba Na yanga... Haitoshi mpira ulipoisha ukaendelea kukaa kwenye hilo hilo banda, mwenye banda akakufukuza.Ukajiuliza niende nyumbani Au nisiende Akili ikakutuma kulala vyumba vya wageni yaani "Guest Houses" Kwa sababu hela unayo unaamua kulala, Au unaamua kwenda kwa rafiki yako kulala huko. Au kila unapopata nafasi ya kurudi nyumbani basi unarudi ukiwa mnyonge sana tena mnoo. Maana unajua utamkuta mkeo hajalala na kawaka ile vibaya sana, Kiufupi hauna AMANI na FURAHA toka umeoa. Huenda umewahi kumsomesha binti ghafla alipokaribia kumaliza masomo yake Chuoni Au Shule. Akabadilika na kusema "...Ahsante kwa kunisomesha mimi nilikuwa nakuchukulia kama kaka yangu..."
Kitabu hiki kitakufanya maisha ya aina hiyo kuwa historia kwako.