SAFARI YA MAFANIKIO
Katika utafutaji wowote wa mafanikio hauwezi kukosa vikwazo mbalimbali ambavyo vinaweza kukudanganya na kukuaminisha kwamba mafanikio ambayo unayasaka sio kwaajili yako lakini kumbe kuna vitu nyuma ya safari yako ya mafanikio unatakiwa kuvitambua ili unapokutana na changamoto na vikwazo mbalimbali ujue vinamaanisha nini kuhusiana na safari yako ya mafanikio.
Kila mmoja anahitaji mafanikio, lakini sio kila mmoja anayethubutu kupambana ili kupata mafanikio ambayo anayahitaji kutokana na kutokuelewa safari yake ya mafanikio inavyotakiwa kuwa. Safari yoyote ile lazima iwe na maandalizi ili ikusaidie uweze kufika salama kule unakoenda, sio kukurupuka na kuanza safari yenyewe, huku kukurupuka ndiko ambako kunasababisha wengi kutokuingia katika safari hii ya mafanikio yenye matunda mazuri. Safari ya mafanikio huwa na nyakati tofauti pamoja na majira tofauti, katika maisha yetu, kuna wakati safari inaweza kuwa ngumu sana, kuna wakati hata unathubutu kutaka kukata tamaa lakini ukweli ni kuwa sio kwamba ukijiandaa hutakutana na changamoto za kuelekea katika mafanikio yako, changamoto utakutana nazo na zitakusumbua sana kabla hujafika kwenye mafanikio yako.
Cha msingi ni kuelewa unataka nini katika maisha yako na kusimamia msimamo wako.
Kitabu hiki cha Safari ya Mafanikio ikiwa ni toleo la pili katika mwendelezo wa vitabu vya AKILI YA USHINDI, kuna ishara na alama ambazo tumeweza kukuwekea kwa njia ya maandishi kuhakikisha kwamba safari yako inakuwa salama na yenye matunda mazuri. Kitabu hiki kitaenda kukufungulia milango ambayo ilishafungwa na fikra zako, sio hivyo tu bali ninaamini kwamba utakapomaliza kusoma kitabu hiki lazima uwe umeshapata kitu fulani cha kufanya katika maisha yako na hata jamii yako ikanufaika nacho.
“WEWE NI MSHINDI”
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza